SoC04 Matumizi ya Ambulance zinazotumia nishati ya umeme katika kupunguza gharama na kuboresha huduma

SoC04 Matumizi ya Ambulance zinazotumia nishati ya umeme katika kupunguza gharama na kuboresha huduma

Tanzania Tuitakayo competition threads

hiddenb1

New Member
Joined
Jun 7, 2024
Posts
2
Reaction score
1
UTANGULIZI

Kumekuwa na changamoto kubwa sana katika sekta yaAfya hususani kitengo chakusafirishia wagonjwa kwa kutumia Ambulance, hii ni kutokana na gharama ya usafirishaji kuwa juu zaidi na kupelekea matokeo mabaya hata vifo wakati mwingine.

Hivyo basi kutokana na ukuaji wa teknolojia dunia na mabadiliko ya kidigitali nichukue nafqasi kupendekeza hoja ambayo itapelekea upungufu wa gharama za usafirishaji wa wagonjwa utakao sababisha kukua kwa hadhi katikaSekta ya Afya kutokana na ubora katika huduma.

Hoja yangu ni hii: Kuzingatia jambo la ukuaji wa kidigitali duniani kumekuwa na uzalishaji wa magari yanayotumia nishati ya umeme ambapo gharama za kiuendeashaji ni ndogo zaidi kulingana na gharama za uendeshaji magari yanayotumia mafuta.

Jambo hili litapelekea kupungua kwa gharama za usafirishaji wa kwa kutumia Ambulance na kupelekea watu wa aina mbalimbali kuwa huru kutumia magari hayo nakupunguza vifo na athari zilizopo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom