Pole ndugu kwa imani hiyo potofu. Kama nimelielewa vyema swali lako nalijibu hivi.
Asali iwapo imevunwa na kutunzwa vizuri ni chakula kitiacho nguvu mwilini. Limao ni mojawapo ya matunda yalosheheni vitamini. Vyote ni salama mwilini vikitumika vingali bado salama. Aidha asali safi ikichanganywa na limao na haswa ukiongeza tangawizi ni dawa ya kikohozi. Kama kuna ambaye kuchanganya asali na limao vilimgeukia sumu basi zitakuwepo nyingine zikiwemo usafi na afya yake kabla. Mfano, mwenye vidonda tumoni limao litamuathiri kila atumiapo.
naomba msaada Great thinkers,je ni kweli kuwa ukichanganya asali na ndimu/limao inakuwa sumu kwa binadamu?je kuna ukweli wowote wa kisayansi(chemistry)?
Imani imetokea kwa watu wanaosema kuwa mzinga wa nyuki ukiulembea ndimu, nyuki wanakuwa na ghadhabu sana. Hivi kweli umlembee hata kijiwe kidogo tu watakuwachia?. Wanaosema hivi wanadai pia unapochanganya asali na ndimu "reaction yake" inatoa mapovu mengi kwa hiyo ukitia tumboni tumbo litavimba. UONGO. Ukweli ni kuwa asali na ndimu/limau, mbali ya kuwa ni tamu sana, vilevile ni dawa nzuri ya kukohozi, pumu na maradhi yanayohusiana na pumzi.Hii imani imekuwepo sana.Sijui ilitokea wapi
Imani imetokea kwa watu wanaosema kuwa mzinga wa nyuki ukiulembea ndimu, nyuki wanakuwa na ghadhabu sana. Hivi kweli umlembee hata kijiwe kidogo tu watakuwachia?. Wanaosema hivi wanadai pia unapochanganya asali na ndimu "reaction yake" inatoa mapovu mengi kwa hiyo ukitia tumboni tumbo litavimba. UONGO. Ukweli ni kuwa asali na ndimu/limau, mbali ya kuwa ni tamu sana, vilevile ni dawa nzuri ya kukohozi, pumu na maradhi yanayohusiana na pumzi.
siyo kweli kabisa, mie binafsi nimekuwa nikitumia asali na limao/ndimu kwenye chai/maji ya moto kwa zaidi ya miaka sita sasa na sijawai kuwa na tatizo lolote.
Labda kwa kuwa unatumia chaini na majini,wanasema ukichanganya moja kwa moja,inaleta reaction ambayo inavuruga na kukata kata utumbo na kusababisha kifo cha ghafla
Hii imani imekuwepo sana.Sijui ilitokea wapi
Tausi,
Nadhani ni kukosa uelewa zaidi.Ukiangalia dawa za nyumbani ( home remedies) kwa ajili ya kukohoa na magonjwa ya koo wanashauri uchanganye asali na ndimu na hakuna popote utasikia inaleta au imewahi kuleta madhara.
Nimewahi kusikia pia...lakini aliyesema akasisitiza kuwa inategemea ni asali ya nyuki wa aina gani (wadogo au wakubwa). Nimesahau ni ya nyuki wepi hasa ndio inasadikika kuwa sumu kwa binaadamu endapo itachanganywa na asali.
Mimi huwa nipo interested sana na hizi imani za zamani na kujaribu kuangalia busara/funzo/mantiki yake. Ukizifuatilia, nyingi ya imani hizi zina scientfic basis (au tuseme zinaelezeka kisanyansi) hata kama kwa nyakati hizi relevance yake imepungua au haipo kabisa kutokana na maendeleo.