Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Katika harakati za maisha nikakutana na mdada anatokea nchi fulani sitaitaja. Yule mdada alikuwa anakunywa dawa za kuongeza damu, folic acid, vitamin B supplements na nyingine sikuzitambua. Nikamuuliza" wewe ni mjamzito"? Akajibu hapana. Nikashangaa maana najua hizo dawa hutumiwa na wajawazito.
Akaniambia amejipanga kushika ujauzito miezi kadhaa ijayo hivyo anaandaa mwili uwe tayari kupokea mtoto.
Akanambia pia amebadilisha mtindo wa maisha kama vile kuacha pombe, kulala muda mrefu pamoja na kutumia vyakula vyenye mafuta kidogo na visivyochakatwa viwandani. Kwa kweli nilishangaa, sikuwahi kujua kuna watu wana huu utaratibu wa kuandaa mwili miezi kadhaa kabla ya kubeba ujauzito.
Je unadhani ni wakati mwafaka na sisi tuanze kupewa elimu hii na kuifanya sehemu ya maisha yetu? Je utamaduni wetu na mtindo wetu wa maisha vitaendana na watu kuandaa afya zao kabla ya kushika ujauzito?
Asante