Matumizi ya fedha za kigeni serikalini katika kufanya maamuzi

Haika

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
2,347
Reaction score
562
Leo nimepata bahati kumsikia gavana wa benki akiongelea swala la mapato ya taifa. Nilishangaa kumsikia akiizungumzia hio habari kwa umma wa watanzania huku akitumoa fedha ya kimarekani yani dola.
Nadhani yeye ni mtaalamu wa mambo ya fedha na uchumi na amepewa hio kazi kwa kuwa ana utashi wa kutuongoza kufikia uchumi bora zaidi.
Pia huwa nasikia kuwa matumizi ya dola ni kati ya mambo yanayoua uchumi wetu au yasiosaidia kuukuza.
Je ni wapi mpaka wa uzuri au ubaya wa kutumia hizo fedha za kigeni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…