Kwa mawazo yangu naona sahihi ni ON. FOR ingekuwa sahihi kama sentensi ingekuwa hivi:
I would like to congratulate you for achieving (kitendo/verb) this....
Katika sentensi zote mbili kuna watu wawili, anayepongeza na anayepongezwa. Matendo katika sehemu ya anayepongeza ni like na congratulate wakati anayepongezwa hajawekewa kitendo ambacho kingeendana na FOR. Maneno "this great" katika kifungu cha maneno "this great achievement" yanapamba tu nomino/noun achievement (yenyewe si nomino kimsingi) hivyo dhana kuu hapa ni achievement ambayo ni nomino. Kwa muundo wa sentensi nzima ON ndiyo sahihi kwa kuwa inaendana na nomino (noun) badala ya for ambayo ingeendana na verb / kitenzi (nasisitiza kwa mujibu wa sentensi hii).
Wanaojua zaidi watatusaidia.