Matumizi ya HIV Rapid Home Test Kit Yamekatazwa Au?

Marumeso

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2009
Posts
1,410
Reaction score
1,325
Matumizi ya HIV Rapid Home Test Kit Yamekatazwa Au?

◇ Maduka mengi ya dawa hawauzi hizi Kit.

◇ Yale maduka machache yanayouza unakuta wanauza kimachalemachale kama vile wanavyofanya wauza bangi au gongo, ukiulizia ni lazma huyo muuzaji aangalie kulia na kushoto mithili ya mtu anayetaka kuvuka barabara ahakikishe kama kuna mtu mwingine amesikia hicho mnachotaka kuuziana.

◇ Tena unakuta wauzaji walio wengi wanazificha mbali huko na wengine huziweka nyumba za jirani kiasi ukihitaji inabidi hadi aifuate huko. Hapo sasa itabd ungoje kwa muda wa kutosha akaitoe huko alikoificha!!

◇ Wakuu TATIZO ni nini hasa, ni kwamba matumizi ya vifaa hivi bado hayajaruhusiwa hapa nchini au kuna nini hasa kwenye biashara hii?

 
Kuna wakati nikiwatafakali hawa masponsa wa hii miradi naona kabisa wanataka weusi tuangamie kabisa.

Wanaweka pesa mingi sana kwenye madawa ya kufubaza ugonjwa (yani baada ya mtu kuathirika) kuliko kule kwenye kuzuia maambukizi mapya.

Hapa ilitakiwa pesa mingi iende kwenye njia za kuzuia kuenea kwa maambukizi mapya ambayo ndo mengi zaidi.
 
Vipo kibao tu, pesa yako. Pale Kariakoo vinauzwa 5,000 TZS.
 
JE na kwa cku 40
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…