Matumizi ya Kemikali ya Ethanol yanaweza kuathiri ini na kusababisha Saratani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni imewahukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela vijana Watatu kwa kosa la uzalishaji na usambazaji wa pombe kali bandia wakitumia Kemikali ya ‘Ethanol’ isivyo halali

Wahusika hao waliohukumiwa Frank Donatus Mrema, Faham Salim Ngoda na Issa Juma Hassan walitumia kemikali hiyo kutengeneza vileo vikali aina ya K-Vant, Double Kick na Smart Gin, wakabandika stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na nembo bandia za kampuni za bidhaa husika.

Hukumu hiyo imetolewa Jumatatu, Mei 27, 2024 na Hakimu Mkazi Veneranda Kaseko baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka, kuwa umethibitisha kesi katika mashtaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili.

Kusoma zaidi Hukumu hii, bofya hapa ~ Watatu jela maisha kwa kukutwa na kemikali za kutengeneza ‘Smart Gin’, ‘Double Kick’

==================

Yafuatayo ni maelezo ya Kitaalam kuhusu Kemikali hiyo:

Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) anafafanua;

ETHANOL (ETHYL ALCOHOL) inapatikanaje?
Ethanol inaweza kutengenezwa kutokana na malighafi mbalimbali kama vile malighafi za molasses, baadhi ya nafaka na kemikali za viwandani kama vile sulphuric acid, phosphoric acid na acetylene.

ETHANOL inatumikaje?
Ethanol ni kemikali ambayo inaweza kutumika katika kuzalisha bidhaa za viwandani na nyumbani.

Miongoni mwa bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa na Kemikali hii ni pamoja na kutumika kuzalisha kemikali nyingine, kuzalisha dawa tiba na vipodozi.

Matumizi mengine ni pamoja na kuzalisha bidhaa za plastiki, kuua vijidudu na kuhifadhi sampuli hospitalini.

Pia, kemikali hii hutumika kutengeneza vinywaji (pombe), manukato, dawa za kusukutua, n.k.

Aidha, kemikali hii inaweza kutumika kwenye mchakato wa kutengeneza Dawa za Kulevya aina ya Cocaine na nyinginezo.

Madhara ya Ethanol
Mathara ya kemikali hii kwa Binadamu yanaweza kutokea kulingana na namna inavyotumika, umri, kiwango na hali ya afya kwa mtumiaji.

Mfano ikitumiwa kama kilevi kwa kiwango kikubwa, kemikali hii huingia kwenye mfumo wa damu na kuweza kusababisha mtu kupoteza fahamu, kuathiri mfumo wa chakula, kusababisha shinikizo la damu, maumivu ya kichwa, hasira n.k.

Matumizi ya muda mrefu huweza kuharibu ini, kusababisha saratani, kuathiri mfumo wa fahamu na uraibu.

Kiwango cha Asilimia 4-5 cha pombe kwenye damu kinaweza kupelekea mtu kupoteza fahamu na wakati mwingine kusababisha kifo kwa mtumiaji.

Dkt. Anthony Gyunda naye anafafanua
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo wa Hospitali ya Muhimbili (Mloganzila), Dkt. Anthony Gyunda naye amechangia hoja kwa kusema:

ETHANOL ni scientific name for ALCHOL in simple words.

Ethanol is the same alcohol, a compound that can be used for multiple purposes like mafuta ya magari, sanitizers, vinywaji vyote vyenye vileo au vilevi kama wine, bia, gongo, nk.

Kwa vile kinywaji hiki husisimua ubongo, mamlaka huwa zimeweka utaratibu wa kupima kiwango cha ETHANOL au alcohol au Pombe katika vilevi ili kudhibiti utengenezaji wa vilevi vikali vinavyoweza kuathiri ubongo.

Ukitengeneza kinyume na utaratibu uliowekwa ni kosa kisheria maana waweza kuleta madhara kwa watumiaji mfano kupofusha, kuua, kupagawisha n.k

Ethanol chanzo chake ni nini?
Asilimia karibu 90 ya Ethanol hupatikana kutoka katika mazao ya mimea jamii ya nafaka mfano mtama, ngano, uwele, mahindi, n.k.

Taarifa zaidi kuhusu utengenezaji wa pombe na vinywaji vikali visivyovingatia ubora soma haya maandiko:
~ Wanywaji wa pombe kali tuwe makini, kuna pombe kali feki nyingi nchini
~ Pombe feki zimekithiri Moshi
~ Konyagi Feki zaivuruga TBL, yapunguza uzalishaji
~ Wanne wakamatwa kwa kutengeneza Pombe Kali 'Feki' Morogoro
~ Kukithiri kwa wingi kwa pombe fake, Mamlaka imeshindwa kudhibiti?
~ Arusha: Mmiliki wa Baa ya Kipong mikononi mwa Polisi kwa kutengeneza Pombe kali bandia
 
Hivi watanzania wanajua haya madhara maana ni hatari tupu
 
Kuna kampaunfi insitwa acetaldehyde nhii husababisha kutanuka kwa ini mwisho wa siku utapata kansa ya ini, acheni pombe
 
Back
Top Bottom