SoC04 Matumizi ya kuhakiki kiasi cha pesa kwa maneno na uwezo wa kuweza kubadili salio kuwa pesa wakati wa miamala ya simu kufuta kilio cha wengi

SoC04 Matumizi ya kuhakiki kiasi cha pesa kwa maneno na uwezo wa kuweza kubadili salio kuwa pesa wakati wa miamala ya simu kufuta kilio cha wengi

Tanzania Tuitakayo competition threads

tz mickey

New Member
Joined
Apr 23, 2024
Posts
3
Reaction score
4
Utangulizi
Kumekua na kero Kadhaa kwenye matumizi ya simu kufanya miamala ambayo huwa inajitokeza na kuchukuliwa kama changamoto ya kawaida bila mamlaka husika kuchukua hatua kutatua kero .Kwa miaka ya hivi karibuni imeshuhudiwa kuzidi kukua kwa hzo huku mamlaka zikikaa kimya bila kutoa tamko lolote kama ifuatavyo

1. Sehemu ya kuhakiki kiasi cha pesa wakati wa kufanya muamala wa simu kuwa na tarakimu pekee jambo linalo chagiza uzembe ama makosa wakati wa kutuma pesa

Hii ni kero ambayo kwa namna inaonekana ya kawaida lakin kwa jamii ya sasa imeshuhudiwa ongezeko la watu kuwa na hali ya uvivu kwenye kusoma tarakimu .Je serikali au mamlaka husika zina mpango gani kuweza kutumia kiasi cha pesa kwa maneno kuwa kama moja ya njia ya kuhakiki pesa kabla ya kuruhusu muamala wa simu kwenda kwa mtu mwingine

2. Kukosekana uwezo wa kubadili muamala ulio nunuliwa kama salio kurudi kuwa kama pesa mtandaoni

Kwa hali iliyopo sasa kwa mitandao mingi ya simu,utaratibu hauruhusu mteja kama alifanya muamala kimakosa badala ya kutuma pesa kama pesa na kujikuta akituma kama salio imekua changamoto kubwa hasa kubadili salio kuwa pesa na kuruhusu kutuma tenaa imekua ni kero kubwa ambayo na yenyewe haijapewa kipaumbele kwenye utatuzi je mamlaka husika zina mpango gani kuweza kunusuru watumiaji ama wateja na changamoto kama hizoo kuelekea tanzania yenye maendeleo kisayansi na teknolojiaa ama maendeleo ya kidijitali

Faida za kama itatokea mabadiliko katika mambo hayo
1. Kuhakiki pesa kwa mfumo wa kuhakiki kiasi kwa maneno kuta punguza adha ya kuwa na uvivu wa kusoma tarakimu na changamoto kama hizo hivo itaongeza usalama zaidi kwenye matumizi ya mitandao upande wa miamala ya simu kabla ya kuruhusiwa kwenda kwa mteja mwingine

2. Kuweza kubadili salio kurudi kuwa hela ya kawaida kwenye simu pia itasaidia kupungua kwa hasara ambayo wananchi wengi wamekua waki kumbana nayo hasa kipindi cha kufanya miamala ya simu

Hivyo ni vyema mamlaka husika mfano mamlaka ya mawasiliano TCRA na makampuni ya simu zikachukua hatua stahiki kwa ustawi bora wa matumizi ya mitandao ya simu kama sehemu ya kufanya miamala ama kuhusika kwenye mzunguko wa pesa.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom