DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Lugha ndio nyenzo kuu inayotumika kufikisha ujumbe kwa walengwa. Ingawa kuna nyenzo zingine kama picha, michoro, ishara, alama nk zinazotumika katika kufikisha ujumbe lakini lugha ndio nyenzo pekee yenye kueleweka kwa haraka na isiyo na ubaguzi.
Lugha hii inapotamkwa kwa ufasaha na mpangilio mzuri wenye kuzingatia muala, huleta ladha kwa hadhira na shauku ya kutaka kuendelea kukusikiliza. Lugha fasaha ni lugha inayozingatia kanuni za matamshi, muundo, kaida na mantiki katika lugha husika.
Miongoni mwa watu wanaotumia lugha kwa kiasi kikubwa katika kufikisha ujumbe kwa hadhira zao ni viongozi na wahubiri wa dini mbalimbali kwenye majukwaa ya dini iwe katika viwanja vya hadhara au katika maeneo yao ya ibada. Hivyo basi mhubiri anatakiwa awe hodari sana katika kuifinyanga lugha na kuzungumza matamshi yenye ufasaha wa hali ya juu ili kuleta uelewa kwa hadhira yake.
Katika maeneo niliyo bahatika kupita na kuchunguza nimegundua kwenye majukwaa ya dini matumizi ya lugha fasaha hasa lugha yetu hii adhimu ya Kiswahili hayazingatiwi. Jambo linalopelekea mhusika kushindwa kuteka hadhira anayoihutubia. Wakati mwingine hutumia lugha ngeni na isiyofahamika kwa hadhira anayoihubiri. Hivyo kupoteza malengo yaliyowekwa kufikiwa kwa mikutano hiyo au hadhara hizo. Kwani hata Manabii walipelekwa kwa watu wao kwa lugha husika ya hao watu, na wao (Manabii) walikua ni fasaha sana katika kulifikisha neno la Mungu kwa kaumu zao.
Kubwa zaidi kwa hawa wahubiri na viongozi wa dini, hata wanapotafsiri maandiko na kutolea ufafanuzi, utawakuta wakitumia lugha duni na wakati mwingine kwa kukosa maneno fasaha ya Kiswahili hujitumbukiza katika shimo la kutumia maneno yasiyo rasmi na maneno ya mtaani.
Lengo langu sio kuwatweza na kuwasemanga wahubiri wetu, la hasha! Lengo ni kuonesha mahali penye udhaifu na kuangalia namna njema ya kuweza kuondosha udhaifu huo. Hivyo ni matumaini yangu kuwa bandiko langu hili litakua ni chachu ya mabadiliko kwa viongozi wetu wa dini na wahubiri katika majukwaa ya dini. Ni aibu kwa msomi mkubwa wa dini ambae amehitimu ngazi za juu za masomo ya dini lakini akawa hana weledi wa matumizi ya lugha fasaha katika mahubiri yake. Kuna haja kubwa kwa viongozi wetu wa dini na wahubiri wajiendeleze kusoma lugha ya Kiswahili ili waweze kuitambua vizuri. Au wakiwa katika masomo yao ya dini wapewe na kozi maalumu ya matumizi ya lugha fasaha ya Kiswahili.
Hili litasaidia mambo mengi kama haya yafuatayo;-
Ushauri wangu kwa kila mmoja wetu ni kwamba tuendelee kujifunza hasa lugha yetu ya Kiswahili kwani elimu haina mwisho, binadamu anatakiwa awe ni mwenye kujifunza muda wake wote atakaokuwa hai. Sio ujinga mtu kufahamu kuwa hajui na akafanya juhudi ya kujielimisha. Niwashauri wahubiri wote ambao kwenye upande wa matumizi ya lugha fasaha ya Kiswahili ni changamoto, wajiendeleze kwa kukisoma Kiswahili na kukifahamu sawasawa ili wanapokua wanahudhurisha mafundisho ya dini yavutie na yawe na ladha lenye kuakisi kile wanachokilingania.
Hilo sio kwa viongozi wa dini au wahubiri tu, bali kwa kila mmoja ambae anapenda kutumia lugha ya Kiswahili katika maeneo rasmi ahakikishe anazungumza Kiswahili fasaha. Pamoja na waandishi katika mabandiko yao. Lugha ya Kiswahili ni hazina, na kusoma Kiswahili ndio funguo ya kufungua hazina hiyo. Kama sisi wenyewe hatutokipenda Kiswahili chetu hakuna mwingine atakaekipenda. Tupende vya kwetu.
Na;-

- Kuikuza lugha yetu ya Kiswahili
Kila watu wanapozidi kuzungumza Kiswahili fasaha ndivyo lugha hiyo inapozidi kukua. Kwa sababu ndani yake visawe na misamiati mipya huchomoza na kufahamika kwa watu wengi. Kadri watu wanaozungumza Kiswahili wanavyoongezeka ndivyo Kiswahili kinavyokua na kutanuka. - Kuyafanya mahubiri kuwa matamu na yenye ladha kwa hadhira kutokana na matumizi ya lugha fasaha. Na ndio maana maneno ya Mitume na Manabii yalikua matamu sana, na kila aliyeyasikiliza yalimvutia na kumuingia mpaka ndani ya moyo wake. Hii ni kutokana na ufasaha wa Manabii katika mazungumzo yao, ufasaha ambao walipewa na Mwenyezimungu kama karama.
- Miongoni mwa msingi ya sheria za dini, ni kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa weledi na utambuzi wa sawasawa na sio kubahatisha. Hata lugha inayotumiwa na wahudumu wa dini iwe ya uhakika kwa maana iwe lugha fasaha yenye kuendana na kanunia na taratibu za lugha husika.
- Wahubiri kuwa na hadhi kwa hadhira. Kuna baadhi ya watu husema kabisa mhubiri fulani yupo vizuri lakini tatizo sio fasaha katika mazungumzo yake. Hivyo inapelekea watu wakamshusha hadhi/thamani kiongozi wao au mhubiri kwa kuwa tu hana ufasaha katika kuwafikishia watu maneno ya Mungu. Mhubiri mahiri wa lugha aliye mfasaha katika mazungumzo yake na mahubiri yake hadhira huvutika na yeye kwa ufasaha wake tu hata kama hatokua mbobezi katika masuala ya imani na dini kwa ujumla.

Upvote
1