Mafuta ndo chakula chake kikubwa.....ulitaka itumie mtori au mchemsho!!!!
Ukiibana itapungua nguvu, kuanzia speed 100 kwenda juu ndo inakula sana wese,chini ya hapo ulaji ni wa kawaida.hebu twambie inakula lita ngapi kwa kilometa, na kwa speed ipi?
mkuu fafanua vizuri ili tukusaidie suala la gari kutokuwa na return sio ishu hapo coz asilimia kama 80 ya magari ya sasa hivi hayana return.
mkuu labda tukuulize kuwa hiyo gari mwanzo ilikuwa inakula mafuta kiasi gani na sasa inakula mafuta kiasi gani??
kuna vitu vingi sana hapo vya kuangalia kama plug,air clener,nozzel, ignition coil and wire.
je gari haina miss yoyote??
kitu kingine hapo jaribu kucheki oxygen sensor na idle sensor hivyo vikiwa vibovu huongeza uraji wa mafuta
Mkuu sijui uchumi wako lakini maadam umeanza kulalamika kuhusu wese ni wazi utakuwa sio fisadi. Hiyo gari haikufai, fuel consumption hiyo hata VX V8 haioni ndani (7 km/litre). Huo ni ulaji mafuta unaokaribiana na wa Lori. Mafundi wakianza kuchokonoa chokonoa sana wataiharibu. Itumie mara mojamoja hivo au iuze tu. Lakini ni muhimu kuwa na gari yenye hadhi ya jeep home. Inalinda heshima mtaani.