SoC04 Matumizi ya mifumo katika kudhibiti rushwa na upotevu wa fedha na kuleta uwazi na ushirikishwaji kwa wadau

SoC04 Matumizi ya mifumo katika kudhibiti rushwa na upotevu wa fedha na kuleta uwazi na ushirikishwaji kwa wadau

Tanzania Tuitakayo competition threads

nyarubanjagen-a

New Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Karibia sekta nyingi za umma hazitumii mifumo thabiti katika kukabiliana na upotevu wa fedha na rushwa kwa namna tofauti licha ya maendeleo makubwa ya tehama kwa kiasi kikubwa nchini na hata duniani.

Sekta na idara nyingi za umma zinatumia mifumo kwa masula ya kawaida ambayo hayahusiani na udhibiti wa rushwa ama fedha za umma katika maeneo mengi kama rushwa za Barabarani,ngono na masuala ya ununuzi na kandarasi kwa ngazi tofauti.

Kutokutumia mifumo kunaisababishia serikali kupata hasara ya upotevu wa fedha ,kukosekana kwa uwazi lakini pia kukosekana kwa uwajibikaji kwa baadhi ya watumishi.Hivyo basi ni vyema kuhamasisha matumizi ya mifumo karibia idara na sekta mbalimbali kama ifuatavyo.

Takukuru iunganishwe na mfumo wa utoaji fedha kutoka hazina ili kudhibiti upotevu wa fedha za miradi.Mfuko wa hazina ukiunganishwa ili kuiwezesha Mamlaka ya kukabiliana na rushwa kuanza kufuatilia matumizi ya fedha pindi tu inapotolewa kutoka hazina kwa ajili ya utekelezaji miradi .Kwa mfano fedha inapotoka hazina kwenda kwenye taasisi basi Takukuru ipate unumbe wa kuarifu (notification).Hii itasaidia Takukuru kuanza kubaini mienendo ya kifedha mapema na kuanza kufuatilia kuliko kusubiria hela ikatumike ndo waanze kuchunguza na kwa hivyo mfumo wa wa uperepembaji na tathmini uanze pale pesa inapotolewa hadi site kwenye miradi unapotekelezwa na kila hatua ya mradi Takukuru ihakikishe inajiridhisha na Kwa kufanya ivo itasaidia kubaini mapema uchepushwa wa fedha za miradi.

Wadau wawezeshwe mfumo wa akili mnemba ambayo itasaidia kuwaongoza katika kutoa taarifa za tukio mapema ili kukabiliana na rushwa ya ngono :Uwepo Mfumo wa unaomwongoza mlalamikaji ambao utakuwa unapokea taarifa zake za awali na baaada ya hapo Takukuru ianze mara moja kumwezesha mlalamika kusaidia upatikanaji wa wa ushaidi wa picha /video na hata jumbe na simu zilizopigwa na wahusika wote wawili kwa ajili ya kurahisha ushaidi usio tiliwa , kwa mfano endapo ikitokea muhanga wa rushwa.ya ngono basi mhusuka atahitajika kupata huduma ya mfumo kwa njia ya mtandao ,( online ) na kwa kawaida kupitia menyu iliyo ya kawaida kamba ambavyo inafanyika kwa menyu ya huduma za kiserikali kwa kupiga *152*00#.09.(Rushwa).

Zabuni za ununuzi na kandarasi zote ziundiwe mfumo wa pamoja bila kujali ni ndogo ama kubwa.Tender zote zinazohusiana na shughuli za kiserikali zitangazwe na kuombwa kupitia mfumo mmoja ambao utaratibiwa na idara kama mamkaka ya udhibiti ununuzi wa umma (PPPD) na hivyo kila halmashauri ama taasisi yeyote ya serikali inayotekeleza mradi itoe tangazo kwa wadau kwa ajili ya kandarasi hiyo kupitia mfumo huo mahususi utakaokuwa ukiratibiwa na idara husika mfano kama ambavyo idara ya ofisi ya raisi sekritarieti ya ajira inavyofanya kwa kutangazi ajira na kuwafanyia usaili wahusika na kisha kutangaza waliopata hizo nafasi ndivyo hivyo hata tenda zote zitangazwe na idara hiyo teule na taasisi zote zenye miradi ziweze kutoa tangazo kupitia mfumo huo vivo hivyo hata kwa mfumo wa TANEPs endapo ukifanyiwa marekebisho ya kisheria na maboresho ya kimfumo .Hii itasaidia kuongeza uwazi na kudhibiti ukiukwaji wa taratibu za manunuzi lakini pia itasaidia upatikanaji wa taarifa za tender kwa wadau mbalimbali na kufanya kuwaondolea usumbufu wa kutafuta tender za serkali.

Mwongozo wa uaandaaji bajeti uwe wa kidigitali zaidi : Kutokana na ukweli.kwamba si watu wote wanashiriki katika mikutano ya hadhara ili kupendekeza vipaumbele vya bajeti kutokana na sababu nyingi kama vile kuugua,majukumu ya kikazi ,hivyo ni vema kuwa mwongozo wa uuandaji bajeti ukaboreshwa ili kurushu hata yule asiyekuwepo kwa mkutano kutoa vipumbele vyake kwa mfano mkutano unapofanyika siku husika ni vyema mtu asiyeweza kufika katika eneo husika akatoa maoni yake kwa mtaa ama kijiji anachotokea kupitia mfumo na kisha maoni yake yakahifadhiwa kwa ajili ya maamuzi kwa ngazi inayofuatia kwa kata na kutofautisha asiyehudhuria mfumo utamtaja kuwa mhusika aliyeshiriki kwa mtandao na aliyepo eneo husika utasomeja kama physically attendant.Hii itasaidi kuongeza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali haswa vijana ambao mara nyingi hawahudhirii mikutano hiyo na kufanya vipaumbele vyao kutofikika kwa waamuzi wa sera.pili itasaidia upatikanaji wa taarifa sahii kama vile uwepo wa miradi eneo husika unaofadhiliwa na serikali kutokana na mapendekezo ya wakazi wa eneo husika ,tatu itasaidi wadau kama vile wabunge na madiwani kusemea vipaumbele vya wakazi wa eneo husika.

Makusanyo ya ushuru yafanyike kupitia mfumo wa kielektroniki: Wajasiriamali wadogo wadogo watambuliwe kwa kupatiwa vitambulisho maalumu vyenye namba ambayo atakuwa analipa kila anapoenda kufanya biashara badala ya kaujiri watumishi ambao saa zingine hawapeleki fedha kamili .Mfumo ukitengenezwa vizuri utatumika kubaini mjasiriamali x kwa mfano aliyeko mtaa y ametoa kwa kulipia huduma ya ushuru kwenye soko la mbugani kwa siku ya jtatu -jmosi .wanaoajiliwa kwa ajili ya kukusanya ushuru wasihusike kukusanya badala yake kazi yao iwe ni kukagua taarifa za Wajasiriamali ama wafanya biashara ikiwa wamelipa ikiwa yupo sehemu ya biashara na pia waende kutoa elimu tu.

Hitimisho: Ili kuhakikisha haya yote yanafanyika ni vyema watunga sera haswa upande wa wanasiasa waweze kuwa na utashi wa kisiasa wenye kusikiliza maoni ya wananchi wake na kuyafanyia kazi lakini kwa watumishi wa umma ni vyema wakapandikizwa chembe chembe za uzalendo hata kama kwa kuwalazimisha kupitia mifumo ya kisheria ili kuzuia miendelezo ya rushwa kwenye vyombo ama mamlaka wanazotumika na elimu itolewe pia kwa wadau mbalimbali.
 

Attachments

Upvote 5
Back
Top Bottom