Matumizi ya ndizi katika urembo

Matumizi ya ndizi katika urembo

Doncy monco

Member
Joined
Jul 26, 2019
Posts
38
Reaction score
104
Ndizi ni chakula na pia bidhaa muhimu katika urembo.
Matumizi ya ndizi katika urembo
Ndizi zina virutubisho muhimu vinavyoboresha ngozi. Ndizi pia zina aina tatu za sukari zinazojulikana kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’ .

Hakikisha unanawa uso wako mara tatu kwa siku. Unapofanya hivyo unaondoa uchafu.

Ndizi pia husaidia kuzuia chunusi.

Hakikisha unanawa uso kwa sabuni ambayo inaendana na ngozi yako. Ikiwa ngozi yako ni ya mafuta, hakikisha unatumia sabuni ambayo itakuacha ukiwa mkavu na kama ngozi yako ina ukavu, jioshe na sabuni itakayokufanya uwe na unyevu.

Kulainisha ngozi
Changanya asali na ndizi moja iliyopondwa na upake kwenye uso na shingo. Nawa uso kwa maji ya fufutende baada ya muda wa nusu saa. Fanya hivi angalau mara moja kwa wiki

Kung'arisha uso
Ndizi huwa na Vitamin C ambayo husaidia kuiweka ngozi kuonekana iking'aa. Kwenye ndizi iliyopondwa, ongeza vijiko viwili vidogo vya juisi ya limau na upake kwa uso na shingo. Osha kwa maji ya fufutende baada ya dakika 20. Ni vizuri kupaka mchanganyiko huu wakati unapoenda kulala

Kuzuia mikunjo
Ponda parachichi na ndizi pamoja. Paka kwa uso na uoshe baada ya muda. Mchanganyiko huu hulainisha ngozi ya uso na kuwa laini lakini pia upunguza ukubwa wa matundu ya ngozi ya uso wako
 
Back
Top Bottom