Mkuu watumiaji wengi wa neno hilo boreka hutumia kwa maaana ya kuchoka sanjari na neno la kingereza bore.kwa mfano wako wa bora na best,Je kusema X-PASTER ana maisha bora na X-PASTER ana maisha yaliyobestika yote ni sahihi?
Mkuu, mimi nilielewa sana, nini ulikuwa una maanisha, ila lengo langu ni kutaka kuonyesha kuwa neno boreka kwenye lugha ya Kiswahili lipo na lina maana tofauti na hao wanaolitumia.
Waswahili tunao maneno ambayo tunaweza kuyatumia kwa hali kama hii.
Kwa mfano tunaweza kutumia neno
Udhi Mf: Umeni
udhi au Unani
udhi, Kani
udhi, Alini
udhi, au kwa kiswahili cha mtaani; Michosho, mf: jamaa michosho sana yule. (japokuwa neno Udhi kwa kiingereza fasaha ni Annoyance, Disturb, Bore, Grieve,Infuriate, Vex, Worry, Offend, Tire, Harass, or Hurt).
Vile vile kama unataka kutaja mtu ambaye ame bore,
boring person (noun) tunasema: Mchoshi, Mkulivu, Mchovu. au utasema ...jamaa ananichosha tu na mambo yake/simulizi zake.
Hicho ndio Kiswahili, japokuwa tunakiona kama akipendezi pendezi vile, lakini ndio hivyo inavyopaswa kutumika.