Mkuu watumiaji wengi wa neno hilo boreka hutumia kwa maaana ya kuchoka sanjari na neno la kingereza bore.kwa mfano wako wa bora na best,Je kusema X-PASTER ana maisha bora na X-PASTER ana maisha yaliyobestika yote ni sahihi?bora best (cf. boreka; from Arabic)
boreka be improved (improves) (cf. bora; from Arabic)
Ni kiswahili sanifu lakini kamwe haimaanishi kuwa bored na hivyo ni uzembe,uvivu na fikra mlegezo kuendelea kutumia neno boreka tukiwa na maana ya kuwa 'bored'.Kuboreka ni kiswahili sanifu kabisa.
Neno 'bore' lilianzia Chuo Kikuu 'Mlimani' miaka ya mwisho ya sabini na hata mwanzoni mwa miaka ya themanini. Wakati huo mtu akiongea utumbo watu walikuwa wanasema ana'bore' na alitungiwa jina la 'borer'. Neno borer siyo sahihi kwa lugha ya kiingereza, kwani mtu ambaye anawa'bore' watu huitwa kwa kiingereza sahihi 'bore'. Mtu anaweza kusema kwa kiingereza, 'Mr/Mrs/Miss... is a bore'.
Kwa maana hiyo hilo neno bore halitokani na kiarabu wala kutokana na matumizi yake ya sasa siyo sahihi sana kwa kiingereza. Kuboreka ilikuwa na maana ya 'to be bored' kwa kiswahili. Haikuwa kiswahili sanifu ingawa jamii yetu tuliokuwa Chuoni wakati ule tuliikubali hiyo 'terminology'. Lakini sote tunaelewa kuwa kwenye jamii kama za vyuo, mashuleni, jeshini kuna vilugha huwa vinazaliwa na kuendelezwa na hatimaye kukubalika na hiyo jamii. Kwa waliopitia JKT enzi zetu tulikuwa na lugha zetu na misemo mingi tu. Hata hapa jamvini kuna misemo imezaliwa na inakubalika kutumika hapa.
Mkuu, mimi nilielewa sana, nini ulikuwa una maanisha, ila lengo langu ni kutaka kuonyesha kuwa neno boreka kwenye lugha ya Kiswahili lipo na lina maana tofauti na hao wanaolitumia.Mkuu watumiaji wengi wa neno hilo boreka hutumia kwa maaana ya kuchoka sanjari na neno la kingereza bore.kwa mfano wako wa bora na best,Je kusema X-PASTER ana maisha bora na X-PASTER ana maisha yaliyobestika yote ni sahihi?
Huu msamiati kwangu...kwa hiyo mzizi ni '-twafish' ama '-kutwafish'? Nadra sana (eg Rais etc) neno la kiswahili kumalizika bila 'herufi kuu' (vowels).Kwa kuswahili sahihi ni "kukutwafish"
Mfano: 'nae yule ananitwafish!'
Huu msamiati kwangu...kwa hiyo mzizi ni '-twafish' ama '-kutwafish'? Nadra sana (eg Rais etc) neno la kiswahili kumalizika bila 'herufi kuu' (vowels).
Ungetuwekea basi ilo neno kutoka uko kwenye lugha ya Kiarabu, nasi tukalisoma....!Mzizi ni twafish au tafish ukipenda ongeza 'i' mwishoni. Ni namna ya kulitamka tu. Asili yake ni neno la kiarabu. Kama mushkel au walakin wengi huweka 'i' mwishoni, zote ni sawa