Kamusi ya kiswahili sanifu toleo la pili inatambua 'Ndiyo' kuwa ni muafaka. Matumizi ya 'ndio' & 'ndo' yanatokana na kiyeyusho 'y' kuwa na sifa za uirabu hivyo wakati wa matamshi wengi huidondosha.
1.ndiye
2.ndipo
Ndio na ndiyo ni maneno mawili tofauti yenye matumizi tofauti. Ndio ni wingi wa neno ndiye.Mfano,
Umoja- huyu ndiye aliyenipiga
Wingi-hawa ndio walionipiga
Ndiyo ni kinyume cha neno siyo.
Matumizi ya neno ndo siyo fasaha,hutumika kimakosa.
mkuu sasa hivi watu tumeishaanza kujifunza kichina pale (UDOM) we endelea baki na mandio sijui ndiyo yako. na leo "faza" yupo NYK ameenda kuingia ubia na chuo flani hivi tuanze kujifunza "u wanna know wala am saying"Habari zenu ndugu zangu. kuwekua na matumizi makubwa sana ya neno NDIO na NDIYO hapa mjini hata humu jf pia, ningependa kujua kama kamusi inatambua neno NDIO au NDIYO.. pia hata neno "Ndiye" ningependa kufahamu matumizi yake
mfano 1: mwizi wetu ___ yule?(ndo,ndiyo,ndiye,ndio)
mfano 2: ulikua unaulizia kwa mzee flani,___hapa sasa. (ndio,ndiyo,ndipo,ndo)
Nawasilisha
Kuna kiswahili sanifu ni kiswahili cha waswahili...waswahili wengi ni watu wa pwani. Wao hawana neno ndio....badala yake wana neno ndiyo, piya hawana neno jua badala yake juwa, au neno mwambia waswhili husema mwambiya...ina maana kiswahili cha kuzungumza tofauti na cha kuandika
Sawi sana mdau, unajuwa kiswahili halisi ni cha washili.....ambacho idadi nyingi ya wakazi wa DAR ES SALAAM, MOROGORO, TANGA & PWANI huwa kinatunika.....kama unabisha jaribu kuwasikiliza namna ambavyo huwa wanaongeya....na pia hata visiwani huzungumza namna hiyo hiyo...jua ni juwa, ambae ni ambaye.....n.kKweli kabisa maana hata wewe umetumia Piya badala ya Pia...
Jf raha stress tupa kule...
Kamusi ya kiswahili sanifu toleo la pili inatambua 'Ndiyo' kuwa ni muafaka. Matumizi ya 'ndio' & 'ndo' yanatokana na kiyeyusho 'y' kuwa na sifa za uirabu hivyo wakati wa matamshi wengi huidondosha.
Kila siku kukicha naona kama miaka kadhaa ijayo kiswahili halisi au fasaha kitakuwa kikizungumzwa na wageni.Wakati sisi wa lugha hiyo tutazungumza lugha mchanganyiko kwa sababu mtu anaongea neno moja la kiswahili linalofuata kingereza na baadae tunaelekea kichina sasa maana mmmmmmh!