Matumizi ya neno "toka"

Chagga King

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
1,866
Reaction score
1,076
kumekuwa na matumizi mabaya Sana ya hili neno "toka" hasa pale linapomuashiria mtu ahame ndani aende nje, unakuta mtu yupo ndani alafu anaambiwa "toka nje" ikimaanisha atoke ndani na aende nje, hii huwa siyo sahihi kabisa.

kwani mtu akishakuwa ndani huwezi muambia tena toka nje, neno toka nje Lina maanisha mtu atoke nje na aende ndani, na siyo atoke ndani alafu aende nje.

unaposema "toka" Ni lazima uambatanishe na sehemu ambayo mtu huyo, anatakiwa aondoke, mf. "toka jikoni" toka bafuni, n.k.
...lakini siyo toka nje wakati mtu yupo ndani.

...najua wengi tumezoea hivyo, lakini embu jaribu kutafakari kidogo, (yaani uache mazoea) alafu tujadili pamoja. Karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…