SoC02 Matumizi ya nishati mbadala baada ya mafuta kupanda bei

SoC02 Matumizi ya nishati mbadala baada ya mafuta kupanda bei

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 2, 2022
Posts
60
Reaction score
75
1. UTANGULIZI
Duniani kote sasa hivi bei ya mafuta hususani mafuta ya dizeli petroli pamoja na mafuta ya taa yamepanda bei na sababu kubwa ikitajwa ni vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Kupanda kwa bei za mafuta mafuta kumesababisha athari mbalimbali za kiuchumi licha ya jitiahada mbalimbali kufanyika za kuzibiti athari hizo. Hivyo basi andiko hili linalengo la kupendekeza matumizi ya nishati mbadala ili kuziepuka athari za kupanda kwa bei za mafuta pamoja na faida za kutumia nishati mbadala.

2. ATHARI ZA KUPANDA KWA BEI ZA MAFUTA
Kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa kumesababisha mfumuko wa bei na kupunguza ukuaji wa uchumi.

(a) Mfumuko wa bei, bei ya mafuta huathiri moja kwa moja bei za bidhaa zinazotengenezwa na mafuta ya petroli. Kama ilivyoelezwa hapo juu, bei ya mafuta huathiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja gharama kama vile usafirishaji, utengenezaji na upashaji joto. Kuongezeka kwa gharama hizi kunaweza kuathiri bei za bidhaa na huduma mbalimbali, kwani wazalishaji wanaweza kupitisha gharama za uzalishaji kwa watumiaji. Kiwango cha ongezeko la bei ya mafuta husababisha kuongezeka kwa bei ya matumizi inategemea jinsi mafuta ni muhimu kwa uzalishaji wa aina fulani ya bidhaa au huduma.

(b) Kupunguza ukuwaji wa uchumi: Ongezeko la bei ya mafuta pia linaweza kukandamiza ukuaji wa uchumi kupitia athari zake kwenye usambazaji na mahitaji ya bidhaa mbali na mafuta. Kupanda kwa bei ya mafuta kunaweza kudidimiza usambazaji wa bidhaa nyingine kwa sababu huongeza gharama za uzalishaji wa bidhaa hizo. Kiuchumi, bei ya juu ya mafuta inaweza kuathiri usambazaji wa bidhaa na huduma ambazo mafuta huzalishwa kwa kutumia mafuta.

3. NAMNA YA KUZIKABILI ATHARI ZA KUPANDA KWA BEI ZA MAFUTA
Athari zinazosababishwa na mafuta kupanda bei za mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa haziwezi kuepukika kwa kuweka vikwazo vya biashara, udhibiti wa bei, na ruzuku. Namna pekee ya kuzikabili athari zinazosababishwa na kupanda kwa bei za mafuta ni kuhimiza matumizi ya nishati mbadala kama gesi pamoja na umeme unaozalishwa na maji au umeme wa jua ambapo serikali ikishirikiana na wataalamu mbalimbali watoe elimu na kusisitiza matumizi ya nishati hizo mbadala.

4. MATUMIZI YA NISHATI MBADALA
Matumizi ya nishati mbadala yanaweza kuwa suluhisho la kuziepuka athari za kupanda za bei za mafuta husuani mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa (Kerosene). Aina za nishati mbadala zinazoweza kutumika ni gesi pamoja na umeme unaozalishwa kwa kutumia maji au mwanga wa jua (Solar Energy).

Ambapo Vyombo vya usafiri pamoja na nyenzo zinazotumika katika uzalishaji zinazotegemea matumizi ya mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa zifungwe mfumo unaotumia gesi au umeme badala ya kutumia mafuta ambayo kwa sasa bei yake inazidi kupanda kilasiku. Kwamfano vyombo vya usafiri vinavyotumia mafuta vitawekwa mfumo maalum unaotegemea matumizi ya gesi badala ya mafuta, au mfumo wa umeme wa umeme aidha umeme wa kawaida au umeme unaozalishwa kwa kutumia mwanga wa jua.

Matumizi ya nishati mbadala yamekuwa yakitumika ambapo kuna baadhi magari pamoja pikipiki zimefungwa mfumo unaotumia gesi au umeme badala ya kutumia mafuta ingawa sio kwa wingi kwa sababu bei za mafuta zilikuwa hazipo juu kama ilivyo kwa sasa. Hivyo basi kwa sasa hivi matumizi ya nishati mbadala inabidi yatumike kwa wingi kwa sababu bei za mafuta husuani mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa zimepanda bei maradufu tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

5. FAIDA ZA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA
Matumizi ya gesi pamoja na umeme badala ya mafuta yanafaida mbalimbali ambazo ni;

(a) Matumizi ya gesi pamoja na umeme wa maji au umeme wa jua kama nishati mbadala kutasaidia kupunguza gharama za uzalishaji kwa sababu upatikanaji wa nishati hizo sio ghali kama ilivyo kwa mafuta ya petroli, diseli pamoja na mafuta ya taa. Hivyo basi bei ya bidhaa mbalimbali au huduma mbalimbali hazitoweza kupanda.

(b) Nishati mbadala zitasaidia katika ujuwaji wa uchumi wa nchi kwa sababu usambazaji wa bidhaa mbalimbali utakuwa unafanyika kwa urahisi hiyo ni kwa sababu nishati mbadala zimepunguza mfumuko wa bei.

(c) Matumizi ya nishati mbadala pia husidia utunzaji wa mazingira kwa sababu nishati ya gesi pamoja na umeme huwa hazitoi moshi mwingi kama ilivyo kwa nishati za mafuta ya petroli, diseli pamoja na mafuta ya taa.

6. HITIMISHO
Serikali kupitia wizara husika ya nishati na madini ikishirikiana na wataalamu mbalimbali itunge sera kuhusu matumizi ya nishati mbadala ili kuziepuka athari za kupanda kwa bei za mafuta hususani mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa na kutoa elimu jinsi gani ya kuzitumia nishati mbadala na kuelezea faida za matumizi ya nishati mbadala katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali au katika utoaji wa huduma mbalimbali zinazotegemea matumizi ya nishati ya mafuta ya petroli, dizeli au mafuta ya taa watumie nishati mbadala ya umeme au gesi katika kufanya uzalishaji au utoaji wa huduma ili kupunguza gharama za uzalishaji na kuzuia mlipuko wa bei pamoja na kukuza ukuwaji wa uchumi wa nchi.
 
Upvote 4

Gas tulio nayo ni moja ya njia mbadala bora kabisa kama ikitumika kwenye mazingira rafiki kwa watanzania
 
Back
Top Bottom