James Godfrey
Member
- Aug 27, 2022
- 19
- 12
MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA KUHIFADHI MAZAO YA KILIMO YANAYO HARIBIKA HARAKA MFANO MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI ILI KUMKWAMUA MKULIMA
Ilikuwa ni jioni moja nimetoka nyumbani kwenda kununua mahitaji kwaajili ya matumizi ya wiki katika soko la mabibo jijini Dar es salaam, lakini baada ya kufika pale nilikutana na hali ambayo iliyinivunja na kuniumiza, iliinichukua dakika kadhaa kutazama jinsi wakulima na wafanya biashara walivokuwa wanahangaika kutafuta namna yakuuza bidhaa zao.
Nyingine zilikuwa tayari zimekwisha haribika nawalikuwa wamesha zimwaga chini tayari kuchukuliwa na wafugaji kama vile wafugaji wa nguruwe ambao kwao ni ahueni amakweli ‘kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi’ kwao ilikuwa ni sherehe sababu mifugo yao imepata chakula lakini ilikuwa ni machungu kwa wakulima hawa na wafanya biashara, wengine walikuwa wanauza kwa bei ya hasara wakiogopa kupoteza vyote japo hata wapate kile walichokitumia kununulia bidhaa hizo au japo wapate hata nauli ya kurudia makwao, baada ya dakika kadhaa za kutafakari ndipo nikapata wazo je hakuna njia ya kumsaidia mtanzania huyu kuepukana na tatizo hili linalo mrudisha nyuma na kushindwa kujikwamua kiuchumi, sikupata majibu la maswali yangu kwa siku ile ndipo nikanunua bidhaa nilizo hitaji kwa siku ile nakurudi nyumbani nikiwa mwenye huzuni, sababu mimi ni mototo wa mkulima ambaye anapitia tatizo hili hili .
Ndipo siku moja nikiwa darasani katika chuo kikuu cha Dar es salaam mkufunzi alikuwa anatufunda kozi ya (FOOD MICROBIOLOGY) iliyokuwa inaeleza namna vyakula vinavyo haribiwa na vijidudu kama bakteria na fangasi,
pia ilikuwa inaeleza jinsi tunaweza kuongeza maisha ya vyakula nakuweza kudumu kwa muda mrefu, ikaeleza baadhia ya njia zinazo tumiwa na mataifa yaliyofanikiwa katika uzalishaji na uhifadhi wa vyakula , matunda na mboga za majani kama vile nchi za India,china,na Afrika ya kusini . ndipo nikakumbuka ile jioni pale mabibo nikajiuliza kwani haiwezekani kufanyika tafiti na kumsaidia huyu mtanzania wa kipato cha chini anayeteseka na tatizo lile lile ,ndipo nikaanzai kusoma machapisho ,
majarida na vitabu mbali mbali vinavyoelezea namna bora yakutunza mazao na kuweza kudumu kwa muda mrefu ,hivyo napenda kutumia jukwaa hili ambalo naamini linawatumiaji wengi hivyo ujumbee huu utaweza kuenea na kuwafikia watanzania wengi ili waweze kunufaika
TATIZO
Yafuatayo ni makosai wanayafanya yanayopelekea bidhaa hizi kuwahi kuharibika
1. UVUNAJI
Ubora wa bidhaa ya mkulima unaanzia tangu siku ile anapoivuna shambani, mkulima inabidi kuzingatia njia bora za kuvuna mazao yao ,zifuatazo ni baadhia ya mbinu bora ambazo mkulima anabidi kuzingatia.
-inabidi azingatie muda sahihi wa kuvuna mazao yake tafiti zinaonyesha katia mda wa asubuhi na jioni ndio bora kwa kuvuna matunda na mboga.
- mkulima aepuke kuweka mazao yake chini kwenye ardhi kwasababu tafiti zinaonyesha udongo ni makazi ya jamii mbalimbali za vijidudu ambavyo vinahusika na kuharibu mazao pia itaepusha michubuko ambapo inakuwa ni rahisi kuvamiwa na vijidudu waharibifu na kupelekea kuoza haraka pia mkulima anabidi kutumi vifaa malumu vya kuvunia kama vile vikapu vyenye matundu madogo madogo yanayoruhusu hewa kupita.
2. USAFIRISHAJI
Ubora wa bidhaa pia unategemeana na namna bora ya kusafirisha mazao toka shambani mpaka sokoni,vitabu mbali mbali vinavyoelezea sayansi ya vyakula vinaonyesha tunda linapokomaa linatoa homoni inayoitwa (ethylene) ambayo inakuwa katika mfumo wa gesi hii ndiyo inayosababisha tunda linaiva na kiwango cha homoni hii kinatofautia kulingana na aina za matunda mfano mrahisi unaweza kujiuliza kwa nini wafanyabishara mfano wa ndizi anapotaka ndizi ziwahi kuiva anaweka ndizi zake pamoja na maparachichi ? jibu ni rahisi ni kwamba parachichi linzalisha kiwango kikubwa cha homoni hiyo ndio maana ndizi zitawahi kuiva ,sasa kupitia sayansi hii ya tunda kuiva tunaweza kuja na majibu mazuri ya njia bora ambazo mkulima atazitumia kusafirisha bidhaa zake.
- Mkulima anabidi aweke bidhaa zake katika vifungashio bora ambavyo vina ruhusu hewa kupita ,pia aweke bidhaa zake kulingana na kiwango cha kuiva aepuke kuchanganya matunda yaliyoiva sana na yale ambayo bado hayajaiva ili kuepuka kusababisha yale ambayo hayajaiva bado nayo kuiva ,pia inabidi atenganishe matunda kutokana na aina asiweke matunda tofauti sehemu moja sababu tuna moja linaweza kusababisha tuna lingine kuiva mapema hivyo kuwahi kuharibika.
3. SOKONI
Hapa inanikumbusha siku moja tulienda na rafiki yangu katika duka moja linalopatikana Mlimani city mle dukani nilifungua jokofu(friji) moja na kukuta boksi limeweka matunda aina ya tufaha(apple) yenye lebo inayoonysha yamezalishwa Afrika ya kusini lebo ile ilionyesha yanaweza kukaa kwa kipindi cha miezi sita bila kuharibika ndipo nilipo mkumbuka wakulima wale na wafanya biashara pale mabibo sokoni siku ile walivyokuwa wanahangaika kuyanusuru matunda yao ambayo hata hayajamaliza wiki tangu yavunwe yasije kuwaharibikia mikononi kabla hawayajauza ndipo nikajiuliza haya matunda yamewezaje kusafirishwa toka afrika ya kusini mpaka Tanzania na yanadumu kwa miezi sita bila kuharibika ndipo nikatanya uchunguzi wa namna bora za kuhifadhi bidhaa hizi ,zifuatazo ni namna bora za kuhifadhi matunda na mbogamboga
NJIA BORA ZA KUHIFADHI MATUNDA NA MBOGAMBOGA
Ili kuhifadhi matunda na mbogamboga kwa muda mrefu inabidi kuzingatia vitu vifwatavyo , moja ni jinsi ya kupambana na vijidudu waharibifu wanaoozesha bidhaa hizi ,namna tutakovyopunguza uzalishaji wa homoni ya (ethylene) ambayo huivisha matunda tunaweza kupambana na vijidudu wa haribifu kwa kuosha vizuri bidhaa zetu na maji safi au na mvuke ili kuodoa na kuua vijidudu hao pia kuhifadhi katika kiwango cha joto na unyevu ambacho kitazuia ukuajia wa vijidudu hivi mfano tunda linapowekwa kwenye friji linadumu mda mrefu sababu katika joto dogo vijidudu hawa wanakua taratibu sana pia kiwango cha unyevu nacho kina changia katika tunda kuharibika hivyo tunapo angalia kiwango bora cha unyevu tunaweza kutunza matunda yetu mda mrefu .
Hivyo kwa kujifunza viwango vinavyo hitajika kutuza bidhaa hii tunaweza kuazisha biashara inayoitwa BIASHARA BARIDI inatumika sana nchi za china na india kwa ufupi hii inahusisha kujenga miundo itakayokuwa na vifaa vya kukontroo kiwangocha joto kiwango cha unyevu na gesi mbalimbali vitakavyowezesha kuhihifadhii bidhaa hizi kwa muda mrefu miundo mbinu hii itajengwa maeneo ya uzalishaji yani mashambani na maeneo ya sokoni, lifwatalo ni jedwali linaloonyesha viwango bora kwa matunda na mboga mboga.
KIWANGO CHA JOTO LA KUHIFADHIA (nyuzi joto)
Karoti (0°C), kabichi (0°C), Nyanya(7-10°C)
KIWANGO CHA UNYEVU WA KUHIFADHIA(humidity)
MUDA AMBAO BIDHAA ITADUMU
Karoti
0
90-95
Miezi 2-5
Kabichi
0
90-95
Wiki 3-6
Nyanya
7-10
85-90
Wiki 4-7
Parachichi
4.4-12.5
85-90
Wiki 2-4
Embe
12
85-90
Wiki 3-4
Nanasi
7-12.5

Upvote
1