Matumizi ya Shower Gel ni yapi?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu,

Nimekuwa nikikutana na hiki kitu kinaitwa Shower gel/body wash kwenye maduka ya vipodozi,nini kazi yake na ina tofauti gani na sabuni ya kawaida ya kuogea?

Na Je jinsia yoyote wanaweza kutumia ? ipi brand nzuri?

Ahsante.



 
Sabuni ya kuogea ya maji. Ni sabuni ya kuogea.
Hazina utofauti zaidi ya kuwa ya kimiminika
 
Ok kwahio matumizi yake ni kama sabuni ya kipande tu?
Ni aabuni kama nyingine ila umuhimu wake kiafya unakuja inapokua matumizi ya watu wengi.

Fikiria uwezekano wa kutumia sabuni ya kupande inayotumiwa na watu wote kuogea bafuni au hata kunawa kwa sabuni ya kipande kabla ya kula unapoenda kwenye mgahawa

Ikiwa gel hakuna mashaka ya kubadilusha uchafu na mtumiaji aliyepita kwa namna matumizi yake yanavyokua
 
Cha zaidi ni safe kiafya compared na sabuni ya kipande kwa familia zinazoshare sabuni bafuni
Sawa,Je ni katika kutoa uchafu zina nguvu zaidi ya hizi za vipande?
 
Asante nimekuelewa
 
Sabuni ya kipande (yabisi), Shower Gel na Body Wash (kimiminika) zote ni sabuni kwa mantiki ya kwamba kazi ya sabuni ya kuogea iwe yabisi au ya kimiminika ni kuvunja vunja uchafu au bakteria waliojilimbikiza juu ya ngozi, nywele n.k

Sabuni za vimiminika mara nyingi hutengenezwa kwa nia ya kutibia/kuleta relief kwa baadhi ya matatizo ya ngozi mathalani pumu ya ngozi au kurejesha unyenyevu juu ya ngozi kwa wale wenye ngozi kavu n.k

Ukiacha hilo, kuna aina nyingi za kuoga mfano kuna bafu passport size hapo ni ndoo ya maji, kopo na lapulapu la kujiswafi, kuna wenye mabafu ya 'bomba la mvua' na kuna watu wenye jacuzzi (yale mabeseni ya kuogea).

Sasa hili kundi la mwisho mara nyingi huwezi tumia sabuni ya kipande, unatumia sabuni za vimiminika
 
Sawa,Je ni katika kutoa uchafu zina nguvu zaidi ya hizi za vipande?
Zinatoa uchafu vizuri zaidi au sawa. Maana zipo pia sabuni za kipande zinasafisha mwili vizuri bila kutumia nguvu nyingi kujisugua.
 
Asante kwa maelezo mazuri
 
Kama wewe huwa unaanza kupaka sabuni kichwani kabla ya kuoga, basi hii haikufai. Huwa inaleta mba kichwani usipotumia maji ya kutosha kujisuuza.
 
Mnabadilishanaje uchafu kwa sabuni ya kipande Ilhali Wanasayansi wanasema kazi ya sabuni ni kuondoa/kuua Uchafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…