AL SADY OLPLANER
JF-Expert Member
- Nov 21, 2016
- 294
- 211
WAFAHAMU WANYAMA WENYE HESHIMA KUBWA DUNIANI.
Katika uumbaji Mwenyezi Mungu aliumba viumbe wa aina nyingi sana, viumbe hao ni pamoja na ndege, samaki wakiwamo na wanyama pamoja na wadudu watambaao na kuruka, pamoja na uumbaji huo viumbe vyote ni binadamu pekee aliyeweza kupewa ufahamu wa kutambua mema na mabaya, kama ambavyo mwenyezi Mungu alivyowapa daraja la juu binadamu, imekuwa vivyo hivyo na kwa wanadamu ambao nao kama walivyopewa daraja la juu, na wao wamekuwa wakijaribu kuvipa heshima ya daraja kubwa viumbe wengine ambao hupatikana katika mataifa yao, katika chapisho hili nitakuonesha baadhi ya nchi na mnyama ambaye wao wamempa heshima kama Taifa.
1 Australia mnyama wao ni Kangaroo
Upekee wake ni kwamba mbali na uwezo alionao wa kuamuamua azuie mimba na azae kwa wakati ataopenda, lakini anapatikana Australia na Guinea tuu.
2. Uberigiji wao karata yao ni kwa Simba.
Pengine uhodari na ushupavu wa mnyama huyu ndio uliwapendeza kumpa heshima kubwa hiyo.
3. Kwa Kanada Panya buku na Farasi ndio waheshimiwa.
Hivyo yakupasa ujue wakati wewe unadharau hiki, ni hicho hicho kwa wenzio ni lulu, isikustaajabishe kwa Panya buku ni viumbe waelevu na wenye akili mfano mzuri ni chuo cha sokoine hapa nchini ambapo buku hutumika kupima ugonjwa wa Tb, na hata sisi ilitupasa tuwafanye hawa kama kanada maana wapo hadi ambao mgongoni wana rangi za bendela ya Taifa.
4. Nchini China wana Dragon
Nyoka mkongwe na wa asili ambaye ana miguu minne, anapewa heshima hiyo kama ishara ya umoja na nguvu kwa wachina, Dragon ni miongoni mwa viumbe ambao kwa huonekana kwa picha tuu, kwakuwa uwepo wake unahusiana na simulizi za kale hususani kuanzia chimbuko la Wachina.
5. Denmark kipepeo na bata maji ndio wamepewa nafasi.
Wanyama takaribani wote huwa na ishara flani kwa mfano kipepeo ni upendo turivu wenye furaha, na nnadhani maisha ya wa Denmark yanafahamika, lakini bata wa majini hao ni wajanja na wasafi.
6. Misri kwa Farao ndege Tai ana heshima yake !
Sifa kuu ya ndege Tai ni ubabe na ulinzi kwa wanaye ! Inawezekana Misri wakawa na sifa hiyo kwani ni miongoni mwa mataifa ya ulinzi mkali kwa Africa.
7. Ethiopia ni Simba
Wao ni kama Ubeligiji na sifa za simba nishazisema pale juu, ukitaka kujua kama wapo sahihi jiulize ni nani aliwatawala Ethiopia ?
8. Ugiriki pomboo ndio kiboko yao.
Nikisema pomboo namaanisha samaki dolphin, kwa anayefahamu sifa za pomboo nadhani atakuabaliana na Ugiriki kwamba uchaguzi wao ni maridhawa.
9. India karata zao ni kwa King Kobra, Tausi, tembo pia na chui !
Mpaka nafika mtamboni hapa sikuwa na majibu kamili kwanini idadi yote hiyo.
10.Mexico Na Ufaransa heshima zao walitoa kwa viumbe wafugwao.
Wakati ufaransa wakimfanya jogoo kuwa mnyama wa Taifa, huko Mexico ni mbwa.
11. Urusi mnyama wao wa Taifa ni Dubu.
Dubu ndio mnyama mkali muwindaji anayeua kwa kurarua tuu, pengine walilipa heshima Taifa lao kwa kuzingatia sifa ya mnyama huyo, kwamba wao si watu wa mchezo mchezo. (Pitia gazeti la Mtanzania wiki ijumaa hii safu ya wanyama utamuona na kumuelewa vyema mnyama Dubu)
12. Uingereza nao ni simba.
13. Uarabuni wanyama wenye heshima ni pamoja Ndege Kozi (Falcon), Ngamia, pamoja na pongoni.
14. Thailand imani yao iliangukia kwa Tembo.
Mnyama mkubwa wa ardhini na mbabe, sina hakika kama Thailand ni wababe wa mapambano ya ardhini.
15. Uturuki wamemwamini Wolf
Kwa Tanzania hatuna mnyama Wolf kwa bahati mbaya, ila ili umfahamu ni mnyama jamii ya mbwa mwitu, wao huwa wakubwa zaidi ni wakali na wana mbio kali sana kuliko bata cheetah, sijui kama walikuwa wana maana ya kuwa namba moja kwa usafirishaji.
16. Tanzania ni ............ Piga kelele kwa Twiga !
Twiga ni mkalimu au sio ! Ni mstaarabu ni mpole, ni mnyenyekevu na Mpenda amani ! Nani alipendezwa kutuchagulia kiumbe huyu ! Jike wa Twiga ni waaminifu (Dada zetu nawaona mmewakirishwa vyema) Twiga dume asione ka jike kanachipukia ! (Si mtoa jina mchepuko ) Twiga ndio mnyama mrefu kuliko wote (ahaa shikamo mlima Kilimanjaro) Twiga ndio mnyama ghari kuliko wote hapo juuu (shikamoo Tanzania, dhahabu na madini yote) Twiga anakula majani mazuri ya juu (Tanzania utasema nini kwa mazao) Ni Twiga huhakikisha ulinzi, usalama na amani kwa majilani zake kutokana na uwezo wa kuona mbali (kumbukumbu ipo sawa tulichangia ukombozi kwa mataifa kibao).
Je ungependa kujua Mengi kuhusu wanyama ! Fanya hivi weka comments hapo
Karibu tufanye utalii wa ndani pamoja !
Wasalaam !