Baba Swalehe
JF-Expert Member
- Jun 6, 2017
- 20,178
- 39,641
Tunaendelea na mada zetu za afya ya akili ambapo leo tutaangalia jinsi simu zinavyoathiri mfumo mzima wa akili na jinsi jamii inavyopeteza uwezo taratibu bila yenyewe kujijua na nini kinaweza kufanyika .
Tupo sasa katika ulimwengu wa kiteknolojia ambapo simu zimechukua nafasi ya vitu kama vile camera , redio saa , kalenda na hata vitabu na muda sio mrefu simu zitachukua hata nafasi ya ubongo , kwa sababu watu watakua hawafikirii tena kwa kina ila kila kitu itakua ni kukimbilia kwenda google kuangalia kwa kupitia simu zao .
Tafiti zinaonyesha kwamba watu wengi hutumia kila baada ya dakika nne kujihusisha na simu zao na kufanya vitu kama vile kujibu jumbe fupi , kupokea simu au kuperuzi na vitu vingine vingi vihusianavyo na simu , wengi wetu hata kama hakuna notification tutachukua simu na kuangalia chochote kama kuna message imeingia au hakuna au tutaingia kuangallia kitu chochote kile na hii ni moja ya dalili ya uraibu wa simu za mkononi kama ilivyo kwa pombe na vitu vingine na ukikosa kupata mambo ya mtandaoni kama vile instagram wengine hupata hasira na sonona hivyo kushindwa kufanya kazi zingine .
Madhara ya simu katika afya ya akili ni mengi tutayaangalia kwa uchache sana na nini kifanyike ile jamii iweze kukomboka katika tetemo kubwa linalokuja .
Tukianza na kifizikia simu hazitoi mionzi ambayo inaweza ku haribu ubongo wa binadamu kama wengi wavyofikiria au waliaminishwa katika hadithi mbali mbali za mtaani mionzi ya simu ipo katika ngazi ya ndogo ya mionzi( kwa lugha ya wenzetu huitwa low level non ionizing radiation ) kuweza hata kuharibu vinasaba vya mwili DNA , ila sasa madhara ya kutumia simu kupitiliza ni kwamba huleta kukosekana kwa uwiano sawa wa kemikali katika ubongo wa binadamu , katika maada zilizopita tuliona kwamba katika ubongo wa binadamu kuna kemikali mbali mbali ambazo zingine huleta furaha zingine maumivu na zingine nyingi na madhara ya ukosefu wa uwiano ni makubwa sana .
Matumizi ya Simu kupitiliza hupunguza kwa ujumla uwezo wa ubongo wa mtu kufikiria na kutatua changamoto zingine zilizopo katika maisha , kadri siku zinavyokwenda na tunavyotegemea taarifa zote kutoka kwenye simu tunapunguza uwezo wetu wa kiasili wa ubongo kutatua matatizo , unapotatua tatizo lolote mfano unafanya hesabu bila kifaa cha msaada nyuroni zilizopo kwenye ubongo hufanya miunganiko zenyewe kwa zenyewe kwa ufupi ni kwamba ubongo unakua unafanya mazoezi tofauti na kuupa kila saa taarifa ambazo zinafanya ubongo usitumie nguvu , sikatai simu ni nzuri zinaturahisishia mambo mbali mbali lakini matumizi yake yakizidi mtu hushindwa hata kufanya hesabu ya mbili mara nne mwenyewe kiufupi unakua mzembe sana
Matumizi ya simu kupitiliza kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii kila saa huleta hali ya kutokujiamini na kuona labda umechelewa kufanya maendeleo na kwamba upo sana nyuma ya muda hii inaweza kupelekea kupata msongo mkubwa wa mawazo , unapita huko unakuta mtu kapost anakula kuku kavu na wewe hujala miezi minne unaumia pengine unaanza kujenga na chuki kwa huyo mtu kitu kikubwa ambacho watu hawafahamu ni kwamba kila mtu kwenye mitandao ya kijamii hupenda kuonyesha kwamba ana furaha ila ukweli huwa sio hivyo watu wana mawazo sana mtu utakayemwona amepost anaendesha hammer huwezi jua ana mkopo wa sh ngapi huko kwa hiyo kwa nini ujipe mawazo na upoteze uwezo wako wa kujiamini ?
Pia matumizi ya simu yamepunguza ile hali ya kushirikiana kwenye jamii mfano unatoka kazini unapitiliza moja kjwa moja kutumia simu yako hukai na watoto kuwauliza habari za shule hukai na majirani kuongea kuhusu mambo mbali mbali yanayotokea kwenye jamii husika ikuzungukayo
Matumizi ya simu kupitiliza kutokana na ukosefu wa uwiano wa kemikali mwilini hupelekea mtu kukosa usingizi kwa muda mrefu na sisi wataalamu wa afya huwa tunashauri mtu apate usingizi wa kutosha ili aboreshe afya yake ya akili , ukosefu wa usingizi huweza pelekea mtu kupata sonona na sonona tumeiangalia sana kwenye mada zilizopita , mtu anakosa usingizi hivyo mchana anashindwa kufanya kazi zake kwa umakini na ajabu ni kwamba hata huko kazini atashinda kwenye mitandao na jana kashoinda mpaka usiku wa manane kwenye simu au televisheni
na mwisho kabisa ni ajali za barabarani .
Je tufanye nini sasa kama wewe upo na uraibu wa kutumia simu kupitiliza , hatuwezi sema tuache kutumia simu kwa sababu simu zinaturahisishia wanadamu kazi mbali mbali ila tunatakiwa tujifunze namna ya kuishi na hizi simu na vifaa vingine vya kiteknolojia , kama upo kwenye uraibu kitu cha kwanza unaweza fanya ni kuzuia baadhi ya taarifa ambazo application huwa inakuletea mfano sio lazima kujua kila saa kwamba baba swalehe amependa picha yako instagram sababu ukienda kule utatumia muda mwingine kuangalia vitu vingine , pia unaweza kutenga muda wako wa siku maalumu kwa ajili ya kupita kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii, ukishindwa kabisa itabidi utoe baadhi ya application zinazokutinga kwa muda na uzirudishe pale ambapo unaona kwa sasa unaweza kuzitawala.
Katika saikolojia mbinu mojawapo kubwa huwa inatumika katika kuondoa uraibu wa mtu ni kubadilisha kile kitu alikua anafanya kwa muda mrefu na kitu kingine mfano unaweza badilisha tabia yako ya kutumia simu kwa muda mrefu na ule muda unautumia kwa vitu vingine mfano kusoma vitabu , kucheza na watoto kuongea na ndugu na majirani au kufanya mazoezi
Mwisho kabisa niseme kwamba matumizi ya simu kupitiliza inaweza kuwa ni ishara mojawapo kubwa ya matatizo ya akili na unatumia simu kujiliwaza hivyo LINDA SANA UBONGO WAKO NDIO UNAOENDESHA KAZI ZOTE ZA MWILI PANGILIA VIZURI MATUMIZI YAKO YA SIMU
usisahau kupigia kura makala hii nzuri .

Upvote
13