Ikiwa suala la ajira limeendelea kuwa changamoto kubwa sio tu nchini bali pia nchi jirani, ni wazi kua kujiajiri imekua fursa pekee kwa vijana kujipatia kipato.
kwa bahati nzuri tumejaaliwa vyanzo vingi vya maji ambavyo vinatupatia mazao ya majini ikiwamo samaki.
Wavuvi wadogo nchini wamekua nyuma sana katika matumizi ya teknolojia mpya zinazoibuka kila uchao, hali ambayo inahatarisha usalama wao katika shughuli zao za uvuvi ambazo mara nyingi hufanyika usiku na katika mazingira magumu.
Imesikika mara kadhaa utekaji ukitokea na wavuvi kuporwa mali zao na kujeruhiwa, pia kushambuliwa na mamba pamoja na kuzama kwa mitumbwi. Hapo ndipo swala la utumiaji wa teknolojia ya mawasiliano linaweza kubadili hali ya mambo kwa kiasi kikubwa kwa kurahisisha upatikanaji wa taarifa na msaada wa haraka.
Miongoni mwa hatua zitakazo changia kutatua tatizo hili ni hizi zifuatazo:-
Picha: Baadhi ya mali zilizoporwa na majambazi ziwa Tanganyika kutokea Congo (2014). Chanzo: kigomalive.wordpress.com

- Kuhamasisha utumiaji wa simu za mkononi kwa wavuvi waliopo katika eneo la kazi, hili linaenda sambamba na kuhakikisha kua kuna mawasiliano baina ya wavuvi wote katika eneo husika ili kutoa msaada kwa wenzao pindi dharura itakapo tokea.
- Kutumia teknolojia ya 'radio call'. Ni mfano wa mawasiliano yanayotumiwa na polisi ambayo yanaufanisi zaidi ya simu za mkononi katika maeneo ambayo mtandao wa simu haupo imara. Si polisi tu, bali teknolojia hii hutumiwa sehemu tofauti tofauti mfano makampuni makubwa ikiwemo bandarini na makampuni ya ujenzi. Teknolojia hii itahitaji gharama kidogo za kununua vifaa na kuunda kituo Cha muongozo (Radio Control Station) katika sehemu husika ambazo kwa ushirikiano wa wavuvi hazitokua kubwa sana. Pia, msaada kutoka TCRA ili kufuata taratibu zote za kisheria na kutumia 'frequency' zilizoruhusiwa pamoja na mafunzo ya kuendesha mitambo hiyo ni jambo la msingi zaidi.
- Kutengeneza mfumo utakao ratibu shughuli zote za uvuvi maalumu kwa ajili ya wavuvi wadogo na kusambaza elimu juu ya mfumo huo kwa wahusika. Utengenezaji wa mfumo huo sio swala gumu kwasababu tayari kuna vijana wa kitanzania waliopo vyuoni na waliohitimu wenye uwezo mzuri katika maswala ya mifumo.
Picha: Baadhi ya mali zilizoporwa na majambazi ziwa Tanganyika kutokea Congo (2014). Chanzo: kigomalive.wordpress.com
Upvote
2