SoC02 Matumizi ya teknolojia ya viumbe hai wadogo (Bacteria na Archaea) katika uchimbaji madini katika kutunza mazingira na viumbe hai

SoC02 Matumizi ya teknolojia ya viumbe hai wadogo (Bacteria na Archaea) katika uchimbaji madini katika kutunza mazingira na viumbe hai

Stories of Change - 2022 Competition

Mabula marko

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
44
Reaction score
38
DIBAJI
Shughuli za binadamu zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku kulingana na mahitaji ya mwanadamu kuongezeka , hali hiyo kwa namna moja ama nyingine imekuwa ikisababisha ama kupelekea uharibifu juu ya ardhi na kusababisha uharibifu wa mazingira na kuhatarisha baadhi ya jamii ya mimea kama kiumbe hai kupotea kabisa katika ardhi au mara nyingine kuwa katika hatari ya kupotea

Uchimbaji madini ni moja ya shughuli ambazo mwanadamu hufanya ili aweze kupata kipato kitakachomuwezesha kuendesha maisha yake ya kila siku, shughuli ya kuchimba madini hujumuisha ukataji miti ,ufukuaji wa ardhi ,utumiaji wa maji pia katika nchi zinazoendelea hufanywa kiasilia hasa katika nchi ya Tanzania hufanya kwa njia asilia hasa kwa wachimbaji wadogo hufukua ardhi na kisha kuacha mashimo makubwa hali ambayo huhatarisha maisha ya watu na pia hupelekea mimea na baadhi ya viumbe hai kupotea au kuwa katika hatari ya kupotea

Matumizi ya viumbe hai wadogo katika uchimbaji madini ni teknolojia ambayo inasimama kama suluhuhisho na njia mbadala ya uchimbaji madini asilia , kutumia viumbe wadogo hutunza mazingira na ina usalama kwa watumiaji , mazingira na viumbe hai na pia viumbe hai wadogo wanaweza pia kutumika kusafisha tindi kali zilizo wahi tumika na kuhatarisha eneo hasa maeneo ya migodini

Maneno mhimu; viumbe wadogo, uchimbaji , mazingira , madini na viumbe hai


UTANGULIZI
Uchimbaji wa kutumia wadudu wadogo ni kitendo cha kuchimba madini kwa kutumia njia ya asili ambayo hutegemea muingiliano wa kiasili kati ya madini na viumbe hao wadogo ambao mara nyingi hutumia kuchimba madini yenye thamani kubwa kutoka katika jiwe asilia la madini viumbe hao huwa ni bacteria na archaea (AngloAmerican 2022)

Madini ambayo mara nyingi huchimbwa kwa msaada wa wadudu hao ni kama vile dhahabu, Copa ,Silver , Cobalt , Uranium ,Zinc na Nickel na mara nyingi aina hiyo ya viumbe watumikao niThiobacillus thiooxidans and Thiobacillus ferrooxidans lakini kuna wengine kama pseudomonas fluorescens, pseudomonas putida , achromobacter,bacillus licheniformis ,thiobacillus thermophilica na sulfobus acidocaldarius(Dr.neeraj kumar)
Hii ni picha inayoonesha namna teknolojia hii (AngloAmerican2022)

View attachment 2303453

Njia hii imekuwa ikitumika sana katika uchimbaji wa madini hasa katika maeneo ambayo madini yake hupatikana kwa uchache katika udogo yaani yakiwa yametawanyika tawanyika sana (asilimia ndogo) katika udongo na vile vile kuvuna madini katika mabaki ya udongo katika migodi

Viumbe hai haya wadogo mara nyingi hupatikana katika mazingira ya kawaida hukusanywa kisha kuzalishwa kwa wingi Zaidi katika maabara kwa ajili kukizi mahitaji maana njia hii imekuwa salama kutumika na rafiki kwa mazingira na viumbe hai vyake na kwa Africa tayari imeshaanza kutumika katika nchi kama Uganda na Afrika ya kusini


NAMNA YA UFANYAJI KAZI WA VIUMBE HAWA WADOGO
Kuna njia mbili ambazo hutumika kama ifuatavyo
Njia ya moja kwa moja mara nyingi hutumika na viumbe wenye uwezo wa oksidi chuma chenye sulfa kwa njia ya moja kwa moja electroni kutoka kwa kupunguzwa kwa madini mara nyingi njia hii hutumika na bacteria kama thibacillas(Dr.Neeraj Kumar) ambapo viumbe hukutana moja kwa moja na udongo wenye madini kisha enzemu walio katika bacteria kutenganisha madini na udongo wenye madini(AngloAmerican)​
View attachment 2303460

Njia isiyo ya moja kwa moja katika njia hii viumbe hawa wadogo hawakutani moja kwa moja na udongo wenye madini wakati wa mchakato hivo hutengeza chembe chembe (kemikali) ambazo hutumika kuchakata udongo huowenye madini(AngloAmerican),kemikali hizi hugusana na madini chhuma au protoni yenye sulfa na kupelekea kuwa na kimiminika chenye mchanganyo wenye madini chumana sulfa kama inavyooneka (Dr.Neeraj Kumar)

View attachment 2303465


NJIA ZA KUFANYA UCHIMBAJI KWA KUTUMIA VIUMBE WADOGO
kuna njia mbali mbali ambazo hutumika katika kuchimba madini kwa kutumia viumbe wadogo katika kuchimba madini kama ifuatavyo. Njia ya kuweka Lundo njia hii hutegemea kutengezwa malundo ya udongo wa madini, katika njia hii mchanganyiko wa viumbe hai hao wadogo hunyunyuziwa katika lundo hilo na baadae kukusanya mchanganyiko wa udongo wenye madini na kimiminika chenye wadudu ambao tayari wameshagusana na madini hayo na njia hutumika sana kuvuna madini katika lundo ambayo ni mabaki katika machimbo ya madini (katika Kiswahili kisicho sanifu huitwa Masenga) picha na (medcraveonline.com)

IMG_20220725_111202_758.jpg



Njia ya mteremko kwa kutumia njia hii udongo hutengezwa mdogo mdogo sana kwa kusangwa ama njia nyingine na kisha kukusanywa katika mfumo wa mteremko na kisha kimiminika chenye wadudu hunyunyuziwa katika udongo huo na kisha baada ya muda mchanganyiko wa kimiminika chenye wadudu na udongo hukusanyika chini(AngloAmerican), picha chini na (B.D.PANDEY)

IMG_20220725_115001_926.jpg


Njia ya kuchimba madini ndani ya ardhi katika njia hii udongo wa madini huwa upo katika aridhi katika sehemu yake ya kawaida na kisha kutoboa sehemu zitakazoweza pitisha vimiminika vyenye viumbe wadogo mara nyingi bacteria aina ya thiobacillus kufika mahali madini hayo yalipo baada ya hapo kimiminika hicho hurusu wadudu hao wadogo kukutana na udongo wenye madini kisha baada ya hapo kimimika hicho ambachoa ni muunganiko wa wadudu wenye madini hutolewa nchi na kisha kuchakatwa na kutoa madini(AngloAmerican), picha chini na (medcraveonline ) na (AngloAmerican)

bioleaching-definition-img1.jpg
IMG_20220725_111225_586.jpg



FAIDA YA KUTUMIA TEKNOLOJIA UCHIMBAJI MADINI KWA KUTUMIA VIUMBE HAI WADOGO
Uchimbaji madini kwa kutumia njia asilia huzalisha sumu itokanayo na sulfa dioxide ambayo husababisha matatizo ya kiafya kwa wachimbaji lakini kwa ktumia wadudu wadogo huondoa kabisa tatizo hili
Pia kuchimba kwa kutumia wadudu wadogo husaidia kuondoa sumu zitokanazo na sulphate hivo kuasaidia katika uhifadhi wa mazingira

Vile vile njia hii husaidia kusafisha tindikali katika maeneo ambayo yamekwisha achwa kutumika katika shughuli za uchimbaji na haina madhara katika mazingira kwasababu viumbe wenyewe hukaa katika mazingira hay ohayo na ni rafiki wa viumbe hai na mazingira yake

HITIMISHO
Ukuaji wa teknolojia katika dunia ya leo umekuwa msaada katika kurahisisha na kuweka usalama katika maisha ya binadamu na mazingira yake teknojia hii ni suluhisho ya changamoto ya uharibifu utokanao na mazingira hivyo basi natamani kuona serikali yetu ya Tanzania kuona kama wataanza kutumia teknolojia hii hapa nchini ili kulinda afya za wananchi na kufanya uchimbaji wenye tija kwa utunzaji wa mazingira yake na vile vile uchimbaji endelevu kwa vizazi vya kesho.

KUMBUKUMBU
https:/www.angloamerican.com, Oliver Raymond-barker 2013, uchimbaji madini kwa kutumia wadudu wadogo na Dr. Neeraj kumar channel, B.D.PANDEY, https:/www. medcraveonline.com
 
Upvote 4
Back
Top Bottom