Bususwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2021
- 468
- 1,116
Husika na mada tajwa hapo juu.
Tanzania ni Nchi ya ajabu sana kuwahi kutokea hapa Duniani, Tanzania ni Nchi ambayo bado iko nyuma sana na mambo ya teknolojia.
Tanzania tuna Kitambulisho cha Taifa, maarufu kwa jina la NIDA, Kwa mawazo yangu nilifikiri kwamba kitambulisho hiko kitabeba kila aina ya Kitambulisho kilicho chini ya taasisi za Serikali kuanzia na
1. Leseni ya Udereva
2. Kadi ya Bima ya NHIF
3. Kadi ya mwanachama wa NSSF au PSSSF
4. Kadi ya Mpiga kura
5. Kitambulisho cha kazi
6. Cheti chakuzaliwa
7. Cheti cha Ndoa
8. Cheti cha Darasa la Saba, Kidato Cha Nne na Sita, Chuo Kikuu, Cheti, Stashahada, Stashahada ya Juu Shahada, Uzamili na Uzamivu
8. Mengineyo
Lakini jambo la ajabu kabisa, unakuta mtu anatembea na makadi mengi au kuna kadi kaziweka nyumbani kama vile ni takataka sasa,maana yanakua mengi hadi kero. Hapo bado sijaweka kadi za banks, mfano mtu una account zaidi ya moja kwenye bank,hapo napo pia unakua umebeba kadi za banks zakutosha.
Swali langu nyinyi watu wa serikali, hivi ni kwa nini mmeshindwa kabisa kufanya kadi ya NIDA ikabeba baadhi ya kadi za taasisi za serikali? Kuna haja gani ya mimi kuwa na NIDA,kuwa na kadi ya NHIF,Leseni ya udereva,kadi ya mfuko wa Jamii.kadi ya kupigia kura? Wakati hivi vitu vyote vilipaswa kubebwa na NIDA
Mnakera sana, na mbaya zaidi ikitokea vikapotea hivi vitu,kuvipata kwake ni kazi kweli kweli, mfano upoteze NIDA au Passport ,mambo yako mengi yanasimama.
Tunaomba hili suala lifanyiwe kazi