SoC04 Matumizi ya Vyeti vya Elimu ya Juu kupata mikopo

SoC04 Matumizi ya Vyeti vya Elimu ya Juu kupata mikopo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Rweyemamu Cleophace

New Member
Joined
Jun 4, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Kwa wahitimu wa Elimu ya juu mtakubaliana na mimi kuwa changamoto ya ajira imekuwa tatizo kubwa sana, Serikali, taasisi binafsi wamekuwa wakitafuta njia za kuondosha tatizo ili la ajira.Watu wengi wamehitimu masomo ngazi tofauti lakini baada ya kumaliza ajira zimekuwa ngumu.Taasisi za mkopo zimekuwa ngumu kutoa mikopo,na mwisho wahitimu wameishia kuambiwa ni wavivu, hawataki kujiajili na ikitokea ajira zikatangazwa wanahitaji uzoefu ambao wahitimu hao hawana.

Swali linabaki miaka hii mitatu hadi mitano ambayo huyu kijana anaitumia chuo inamsaidia vipi kujiinua kiuchumi pale anapokosa ajira? Mhitimu huyu anayeambiwa ajiajili anatumia vipi cheti chake kupata mkop?

SULUHISHO: Tanzania tuitakayo tunaomba serikali iweke mazingira mazuri na kuvipa hadhi vyeti vya elimu ya juu viwe msaada kwa wahitimu.

Ni swala la Sera na sheria kutoka kwa serikali na wadau au Taasisi za mikopo, Sera ambazo zinamfanya huyu mhitimu kutumia cheti chake kupata mkopo kwenye taasisi za fedha za serikali na binafsi, Sera ambayo itamfanya mhitimu huyu aone muda alioutumia kusoma kwake una thamani jambo ambalo litaondoa msongo wa mawazo kwa vijana, utaondoa vijana wasio na ajira, Inaweza kuboresha kwa kutamka aina fulani ya GPA kwamba ukihitimu na GPA kadhaa utakuwa na uwezo wa kupata mkopo hii itawafanya vijana kusoma kwa bidii wakijua ikikosekana ajira watapata mkopo, Sharti iwe GPA na wazo la biashara anayotaka kufanya.Wazo ili likiboreshwa na kufanyiwa kazi litakuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi wanaoamini Elimu ndo mkombozi.TUVIGEUZE VYETI KUWA PESA.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom