Kwa mujibu wa taarifa ya TCRA, kwa kipindi cha miezi 3 (July - September 2010) Watanzania walitumia kiasi cha shilingi bilioni 555 kwa kupiga simu na kutuma msg.
Matumizi hayo yalikuwa ni makubwa kuliko mapato ya Serikali kwa mwezi. Kwa mtazamo wangu mahitaji ya simu kwa maisha ya kawaida ni makubwa, lakini haya makampuni ya simu bado yanatuchaji bei kubwa, hivyo ni vizuri sasa bei za simu zikapunguzwa ili kukabili huu ukali wa maisha au wadau mnasemaje?
Hata hivyo sijui hawa TCRA huwa wanaletewa hizi data na makampuni ya simu au wana direct access kwenye database yao. Maana kama wanasubiri kuletewa taarifa, basi itakuwa imeshachakachuliwa ili kukwepa kodi kidogo