Matumizi ya zaburi Dr. Dogoli Kinyamkela 💀 ☠️ 1. Kwa kurudisha mabaya kwa aliyetuma (“Back to sender”)

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,858
Reaction score
5,123
MATUMIZI YA ZABURI
Dr. Dogoli kinyamkela 💀 ☠️

1. KWA KURUDISHA MABAYA KWA ALIYETUMA (“Back to Sender”)
Soma Zaburi 51 mara moja na Zaburi 35 mara tatu kwenye maji. Kata kijiti kimoja cha ufagio vipande vitatu na uviweke ndani ya maji hayo. Kisha kunywa kiasi kidogo na uoge kwa maji hayo kwa siku 3.

2. KWA TATIZO LA KUOTA UNAKULA AU KUJAMIANA KWENYE NDOTO
Soma Zaburi 51, 30, na 69 mara moja moja kwenye maji. Weka na mchanga kidogo kutoka mbele ya nyumba yako. Kunywa kiasi kidogo na uoge kwa maji hayo.

3. KWA KUFUNGULIWA MILANGO YA MAFANIKIO
Soma Zaburi 51, 17, na 30 mara tatu kwenye maji, ongeza chumvi kidogo ya Mawe kisha uoge kwa maji hayo kwa siku 7, kila siku unayasomea maji mapya.

4. KWA KUVUTIA NEEMA NA KIBALI
Soma Zaburi 51, 23, na 3 kwenye maji. Ongeza asali na chumvi, kunywa kiasi kidogo kisha uoge kwa maji hayo kwa siku 3.

5. KWA MSAADA WA HARAKA NA MAFANIKIO
Soma Zaburi 51 na 121 kwenye maji, ongeza sukari au asali kisha uoge kwa maji hayo fanya zoezi hilo kwa siku 7.

6. KWA KUJITAKASA NA KUONDOA VIFUNGO
Soma Zaburi 51, 38, na 69 kwenye maji, ongeza chumvi kidogo kisha uoge kwa maji hayo ndani ya siku 7. kila siku unasomea maji mapya na ndoo ya kuogea usibadirishe.

NB: Mtu Yeyote anaweza fanya haijalishi hauna dini, ni mwislam, budha n. k
 
Huu ni uchawi tu na sio Ukristo watu kuweni macho na mambo haya.
 
Huu ni uchawi tu na sio Ukristo watu kuweni macho na mambo haya.
Tatizo izo bible mnafundishwa juu juu tu hampew na code zake kama izi wanazitumia wao tu Tunatokea sis wenye elim izo tunawafungua maskio unaleta blaah blaah Africa bongo lala sana
 
Hongera sana kwa uzi mzuri tangu nikujue!nitautumia uzi wako vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…