Matunda ni bora kwa mgonjwa wa kisukari ila asile zaidi ya 2-3

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Lishe kwa Mgonjwa wa Kisukari: Matunda ni chakula bora, lakini mengi yao yana sukari nyingi kwa hiyo ni vizuri kula si zaidi ya 2-3 kwa siku ukihakikisha kupunguza ulaji wa zabibu, embe, ndizi mbivu, matunda makavu kama tende, zabibu kavu, zeituni.

Mpaka sasa hakuna dawa ya kuondoa moja kwa moja Kisukari ijapokuwa watu wenye Kisukari aina ya 2, baada ya kurekebisha vyakula wanaweza kujiweka katika hali ambayo mwili unaweza kutumia insulin yake kidogo bila ya kula vidonge au sindano.



Tibafasta
 
Mazoezi pia yanasaidia kuunguza sukari ya ziada. Matunda kama kiwi na parachichi yanafaa.

Ndizi za kijani kama chakula kikuu na kupunguza unywaji wa pombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…