Okhondima
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 1,249
- 1,102
Namna ya kuandaa papai kama mboga.
1. Chagua papai ambalo ni bichi na wala halijaanza kuiva (itakuwa vizuri kama utachagua papai changa)
2. Viungo vingine unavyotakiwa kutumia ni vile muhimu kama NYANYA,VITUNGUU,HOHO,KAROTI na viungo vingine waweza kuongeza kama utapenda.
MAANDALIZI...
A. Osha papai lako na kisha umenye maganda yote pamoja na kutoa mbegu zake.
B. Tumia kikwangulio ama chujio la nazi kulikwangua papai lako ili upate vipande vidogo vidogo kama vile vya kabichi.
C. Andaa nyanya zako,vitunguu,hoho na karoti na kisha uviweke ktk vyombo safi kwa matumizi ya baadaye.
NAMNA YA KUPIKA...
1. Chukua sufuria safi na uibandike jikoni kisha mimina mafuta kiasi na uyaache yachemke.
2. Kaanga vitunguu vyako katika mafuta mpaka vitakapobadilika rangi na kuwa ya kahawia,mimina nyanya na uziache zijikaange mpaka zitakapokauka maji.
3. Mimina papai lako katika nyanya na ukoroge kuichanganya kwa pamoja.
4. Baada ya kama dakika tatu au nne hivi waweza ukamimina hoho na karoti katika mchanganyiko wako, koroga kwa dakika moja kisha tia chumvi na uache kwa dakika 1 nyingine mchanganyiko wako uive.
Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari.Mboga hii unaweza kuitumia kwa kulia ugali au hata wali..
BY OKHONDIMA BUTUPARA.