Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,085
- 4,890
Hakika sasa ni dhahiri watanzania wamejua kwanini hayati magufuli na viongozi wa Mihimili walijiwekea kinga ya kutoshtakiwa.
Nilikuwa najiuliza kwanini wanajiwekea kinga wanataka kufanya kitu gani kibaya kwa watanzania?
Sababu za kujiwekea kinga zimeanza kujulika kupitia spika wa bunge kukiuka kwa makusudi katiba ya nchi kwa kuwakingia kifua wabunge fake 19 waliofukuzwa na chama chao cha Chadema na kuendelea kulipwa mishahara ambayo ni kodi za masikini. Kinachoshangaza Serikali ipo kimya wananchi ndio wanalalamika.
Katiba yetu ipo wazi kuwa mbunge anapofukuzwa uanachama ubunge wake unakoma. Mifamo hai ipo kwa wabunge 8 wa CUF na mbunge wa CCM walifukuzwa uanachama na vyama vyao Spika huyu huyu aliwafukuza bungeni kwa mbwembwe nyingi, leo iweje kwa sifa zile zile za wale wabunge kwanini hataki kuwafukuza wabunge 19?
Tunamwomba rais samia asilifumbie macho suala hili kwani ni ukiukwaji wa katiba unaofanywa na spika kwa makusudi na kuichafua serikali.