Matunda ya Uwekezaji wa Mbowe yaonekana sasa

Matunda ya Uwekezaji wa Mbowe yaonekana sasa

malang0

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
440
Reaction score
523
Matunda ya maono mazuri ya gwiji wa siasa za upinzani nchini (Mwamba) Mh. Freeman Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema kuwekeza kwa Rasirimali watu haswa wasomi vijana leo imekuwa na faida kubwa kwa nchi kutoa viongozi wengi vijana.

Ikumbukwe ni yeye aliyeanzisha mpango wa kutembelea vyuo vikuu mbalimbali mwanzoni wa miaka 2000 na kushawishi vijana kujiunga na chadema. Hakuona shida kutoa fedha na mali zake kuwa-support kisiasa ndiyo maana leo ccm wanavuna kilichopandwa kwa kuteuwa ma-dc wengi waliopita kwenye mikono yake ya uongozi.

Leo baadhi ya Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Ma-dc wengi wamepikwa kwenye mikono yake. Huwezi kumtaja wanasiasa kama Mh. Zitto Zuberi Kabwe, HalimaMdee, Dr. Vicent Mashiji, David Kafulila,Juliana Shoza, Patrobas Katambi, Peter Lijuakali, Prof. Kitila Mkumbo, David Silinde, Mwita Waitara, Cecil M wambe, Pauline Gekul n.k wote kwa sehemu kubwa mwamba kahusika kawapika kisiasa.
 
Tatizo linakuja kuwa wengi wa uliowataja hawana akili nzuri! Na hawapikiki wakaiva!
 
Msaliti kamwe hawezi kuwa mfuasi. Ningekuwa wa kwanza kumpongeza Mr Hai endapo hawa the so-called viongozi magwiji wangekuwa retained vyamani kwao wakiendelea na uanaharakati na ukamanda ili kujiandaa kushika dola.

Au dola hamtaki tena kushika, imebaki kazi tu ya kuwapikia Sisiemu viongozi!??? Basi Sisiemu itakuwa imefanikiwa sana si mchezo, kama mnawapikia na kuwapakuliwa, wao ni kula tu na kuyafaidi matunda ya jasho lenu.

Kwa maneno mengine, ni sawa na nchi za Afrika zinazotumia gharama kubwa sana kuwasomesha raia wake, kisha wanaishia kuyafaidia mataifa ya ughaibuni. Very sad!!!
 
Brain drain theory hii mkuu ya kisiasa ati
 
Back
Top Bottom