Mimi nijuavyo, hundi huwa zinabadilishwa kati ya benki na benki kwenye kitu inaitwa clearing house. Sasa mzunguko wa hundi hizi ambazo zimeandikiwa mfano hapa Dar ni kama ifuatavyo,
tuchukue mfano umepeleka hundi yako JUMATATU imepokelewa na benki husika; kwa vile clearing house huwa kati ya saa tatu hadi saa nne na kuna maandalizi ya kufanya kabla ya kuipeleka kule clearing house, hundi yako itapelekwa JUMANNE asubuhi. Ikifika pale wanampa benki anae paswa kuilipa, mwakilishi huyo anaioanisha against list aliyokuja nayo na kuondoka nayo. Kwa sheria za clearing house, kesho yake siku ya JUMATANO hasipoirudisha kama ina makosa, then ile paying bank in presume kwamba hiyo hundi iko sawa. Hivyo basi hiyo benki inakuwa na obligation ya kuanza kuilipa hiyo hundi kesho yake yaani ALHAMIS.
Kimahesabu yao wanasema muda wa hundi iliyondokwa hapa Dar ni T+3, T ikiwa ni ile siku hundi ilipopelekwa clearing house. Uchelewefu wowote zaidi ya Alhamis ni WIZI MTUPU na UKIRITIMBA usiokuwa na sababu.