Maua Sama na Meneja wake pamoja na Soudy Brown waachiwa kwa dhamana

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Soudy Brown, Maua Sama na Meneja wake(Fadhili Kondo) waachiwa kwa dhamana ya Polisi usiku huu

Watakiwa kuripoti Kituo cha Kati (Central Police) cha jijini Dar walipokuwa wanashikiliwa kesho saa 4

Inadaiwa Polisi walimshikilia mtangazaji Soudy Brown na mwanamuziki Maua Sama kwa kosa la kusambaza video iliyonesha watu wakifanya uharibifu wa fedha za Tanzania

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar, Mambosasa alithibitisha

Ikumbukwe kuwa jana Soudy alipelekwa Mahakamani Kisutu na kufunguliwa kesi moja akituhumiwa kuendesha chaneli ya YouTube ya Shilawadu ambayo haijasajiliwa

Katika kesi ya jana ya Soudy alipewa dhamana lakini alikamatwa tena kwa kesi inayodaiwa kusambaza video hiyo

Habari zaidi, soma=>Jeshi la Polisi linawashikilia Maua Sama na Soudy Brown kwa kudhihaki fedha za Tanzania - JamiiForums
 
Itakuwa wameachiwa kwa maagizo kutoka juu! Pole zao kwa kusota korokoroni...
 
Hivi kurusha maudhui ya kipindi kwenye youtube nayo mpaka isajiliwe!? Kwa mfano mimi labda nilihojiwa live ktk EA Tv, nikaamua kurusha hiyo clip yangu kwa youtube, naweza kubanwa ktk hiyo sheria!?😱😱😱
 
Hivi kurusha maudhui ya kipindi kwenye youtube nayo mpaka isajiliwe!? Kwa mfano mimi labda nilihojiwa live ktk EA Tv, nikaamua kurusha hiyo clip yangu kwa youtube, naweza kubanwa ktk hiyo sheria!?[emoji33][emoji33][emoji33]
Embu jaribu tuone ili tupate jibu la uhakika
 
Ila wamejua oñja joto ya jiwe
 
hao wenyewe ni wanafki, 2020 utawaona mstari wa mbele wanakwambia mama mkanye mwanao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…