Mauaji Wilayani Lushoto, Polisi waache mzaha na uhai wa watu

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kwa zaidi ya wiki nne sasa kumekuepo na mauaji ya kutisha sana wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba zaidi ya Watu wanne wameshauawa kwa nyakati tofauti huku wauaji wakiwapora victims wao except tukio la Jana Mei 23 la kuuawa kwa Mlinzi na wauaji kutokuchukua kitu chochote.

Polisi Lushoto mjini wanachofanya ni kufanya doria ya kuzunguka au kupita mara moja kwa gari yao kisha kurudi kituoni kulala.

Nadhani kwa mtazamo Wangu, Kuna umuhimu wa kutumia Teknolojia badala ya kutumia njia very local za gari.

Hakuna popote hadi sasa imetolewa taarifa kuhusu mauaji haya. Tunaitaka Polisi kuacha siasa kwenye uhai wa watu.
 
Ugumu na kupanda kwa gharama maisha hupelekea kuongezeka kwa matukio ya kihalifu popote pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…