Ukiangalia kwa makini hizi video na hasa wawakilishi wa serikali utagundua matatizo tuliyonayo waafrika. Yaani hatuna hata aibu tunavyoonyesha ujinga wetu.Waafrika kwa ujinga wetu tuko tayari kuwaua waafrika wenzetu, kutetea wizi.Barrick hawalipi kodi pamoja na bei kubwa ya dhahabu!!(kuwa balance sheet yao inaonyesha hasara ndo maana hawalipi kodi)ili tumfurahishe mtu mweupe,Mgeni.Upumbavu huu huwezi kuukuta kwa wenzetu. Hawako tayari kufanya upumbavu ili kumnufaisha mgeni,achilia mbali kuwa mweusi.
Yaani ukisikiliza hata hili swali analoulizwa huyo bwana wa wizara ya Madini, utagundua kuwa huyo mwandishi ndani ya kichwa chake alikuwa anamwambia kuwa "hivi nyie ni wajinga kiasi gani,kiasi cha kushindwa kujua kuwa hapa mnaibiwa"