Mauaji ya Kenya JK na CCM wanaweza kutoa tamko kwa Kibaki?

Ndugu wana JF.
Upande mwingine tuache tu kumsakama Kikwete kuhusu yanayoendelea sasa hivi kwa kutumia tu rungu tu la siasa zetu za ndani. Mkae mkijua kuwa kuna sheria za kimataifa na taifa baina ya nchi na nchi. Sisi tulipokuwa na tatizo la Zanzibar katika uchaguzi mlimsikia Kibaki au Mseveni? Jibu ni hapana. Kuna siasa za ndani ya nchi ambazo rais jirani hana mamlaka ya kwenda na kuwaunganisha majirani katika vurugu kama hii ambayo bado ni mbichi. Kuna taratibu zake. Sasa watu mnaongea ccm, mnataka ccm ifanye nini? Mnataka makamba au mseka au kikwete aende kenya sasa hivi kufanya mikutano na viongozi. Matatizo ya ndani yanamalizwa na wenye nchi wenyewe unless kuna damu ikimwagika sasa mataifa ya nje hayana budi kuingilia lakini kwa kujihadhari. Kikwete asilaumiwe kwa hili. Ameishatoa comment about this drama. Na amekubali kwamba alialikwa lakini kutokana na hali za kiusalama huko Kenya he could not make it. Muwe mnaangalia mifano kama niliyosema pale mwanzoni. When we had problems in Zanzibar who came in Zanzibar to cease the fire? Was that Museveni or Kibaki? The answer is no. Kwa Jumuiya ya Africa Mashariki inatakiwa kutoka ushauri kupitia Mwenyekiti wake Museveni as jumuiya but not individual as Kikwete. Guys tupunguze jazba za kumfanya Kikwete eti silence kwenye hili suala. Manataka yeye aingie stadium ya Kenya kutuliza jazba?
Kikwete has to play a good game there as a president of Tanzania.
 
well said nshomile

you have well elaborated on the "oppose every thing accept nothing mentality".. slowly slowly i hope people will understand
 
Sikuiwai hii thread lakini huko kwenye kenya elections 2007.. progress nilibandika hii, inaendana.


Kwa kweli AMANI!
 
Nashukuru, prof.Tibaijuka na Rais Kufor wameingilia kati, Abbas Gullet wa kenya red cross anahangaika kutafuta chakula na dawa, mama Condoleeza Rice, Ballack Obama na Hillal Clinton wameshaongea na Raila kwa simu aingie meza ya mazungumzo. Tayari NTV wameshaanza kurusha matangazo tangu jana, nimemwona prof.Mathai Wangari akiwasihi wakenya warudie amani.

Tumwombe mungu apishe haya mbali.
 
Nakubaliana na wewe ingawaje hiyo kwenye nyekundu ina matata! Unataka kusema Kibaki alimwalika JK hata kabla hawajatangaza matokeo. Tunaelewea jinsi walivyoharakisha huko. Kusema JK alikuwa anajua hili, ni Hatari tena very serious.
 
Ili ukemee uovu fulani unapaswa kuwa na authority( yaani uwe clean).

(1)Je hivi Jk atanzia wapi kumuonya Kibaki? ikitokea kibakia akwamwabia to hell mbona Nyie huwa mnawaua na kuwaadhibu wananchi wenu mfano akiwekewa video ile ya zanzibar vifaru kibao na mikong'oto kibao kwa wapemba undahani atakuwa humiliated kiasi gani na Kibaki??!!!
(2) Mnadhani Mseveni ana ubavu wa kusema kitu?!!

mmesahau alivyomshughulia Besige huko Uganda?! mmesahu jinsi jeshi livi;ovamia mahakama kuu huo Kampala?!!

Ama kweli watanzania(watu wengine) wana bongo nyepesi za kusahau!!

Give me a break!
 
Nyani hawezi kumhukumu nyani mwenzie, akitoa tamko ikifika zamu yake naye watamtolea tamko, especially kule zanzibar. JK wala CCM hawawezi kutamka. Asalam aleikum
 
Very well said Mkira and that was my point . Tuseme kama hizo sheria za Kimataifa na ujirani zingalikuwa zinampa JK green light angaliweza kusimama kweli na kusema lolote ukizingatia historia ya Zanzibar na Tanzania bara matokeo kutangazwa kwa nguvu tu ?
 
Ni hatari kwakweli! Kikubwa ni kuwaombea tu amani irejee ni ndugu zetu wale.

Hivi Ngombale Mwiru karudi au bado anashuhudia hayo mauaji?
 

Yaani hata kuomba mauaji yasitishwe ni taking sides? Mbona kuna mataifa mbalimbali yameomba vurugu zisimamishwe bile ya kuegemea upande wowote? Kwa kukaa kimya inaonesha tunafurahia mauji yanayoendelea huko.
 
Salaam toka Kenya
Mauaji yemetokea makubwa kisa uroho wa madaraka na mtu kukataa kuitikia sauti na maamuzi ya wanaitaka kuongozwa na huyo anayetaka kuwaongoza kwa nguvu . Watu zaidi ya 700 wamekufa na wanazidi kufa .

Je haitoshi kumuita Kibaki The Hague akajibu mashitaka haya ama ni kipimo gani kinatumika kuwaleta The Hague ?Maana kakataa hata International Community kuingilia na kasema shoot to kill .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…