Mauaji ya Thiaroye, jinsi Waafrika walivyouawa baada ya kuipigania Ufaransa katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Mauaji ya Thiaroye, jinsi Waafrika walivyouawa baada ya kuipigania Ufaransa katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Leo imetimia miaka 80 tangu yatokee mauaji ya askari wa kiafrika waliotoka kupigana upande wa Ufaransa katika vita kuu ya pili ya dunia.

Mauaji hayo yalitokea tarehe 1 Disemba mwaka 1944 katika eneo la Thiaroye nchini Senegal hivyo kupewa jina la mauaji ya Thiaroye( Thiaroye Massacre).

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, kama ilivyokuwa kwa makoloni mengine, baadhi ya waafrika kutoka kwenye nchi zilizokuwa makoloni ya Ufaransa walichukuliwa kwenda kupigana upande wa Ufaransa. Waafrika hao walisaidia kwa kiasi kikubwa kuukomboa mji wa Paris baada ya uvamizi uliofanywa na Ujerumani.

Baada ya kazi ya kuikomboa Paris, waafrika hao walirudishwa Afrika na wakapelekwa eneo la Thiaroye lililopo nchini Senegal. Walipofika Afrika, walianza kudai malipo yao waliyoyategemea baada ya kushiriki katika vita.

Jeshi la Ufaransa lilichukulia madai hayo kama uasi na ndipo ikaamuriwa askari hao waliokuwa wakidai malipo wauwawe.

Idadi kamili ya waliouwawa haijulikani ingawa kuna ripoti zinazodai takribani waafrika 400 au hata zaidi waliuwawa.

Kwa miongo kadhaa, Ufaransa ilitetea mauaji hayo ikidai kwamba ilikuwa sahihi kupambana na "uasi".

Hata hivyo , Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron tarehe 28 Novemba 2024 alimtumia barua Rais wa Sénégal, akikiri kwamba kile kilichotokea kilikua ni mauaji.Emmanuel Macron alichukua hatua hii ili kusafisha jina la nchi yake ambayo imekuwa ikipoteza ushawishi katika eneo la Afrika Magharibi kutokana na kile kilichofanywa na Ufaransa katika makoloni yake, kabla na baada ya makoloni hayo kupata uhuru.

Kutokana na kuchukua muda mrefu kukubali kwamba kilichotokea ni mauaji, nchi ya Ufaransa bado haijawalipa fidia wale waliopoteza wapendwa wao katika mauaji hayo.

VYANZO/SOURCES:
BBC NEWS
FRANCE 24

"Thiaroye killings: France admits West African colonial 'massacre', Senegal President Faye says" Thiaroye killings: France admits West African colonial 'massacre', Senegal President Faye says

000_36ND3GD.jpg
e97ff020-ae4f-11ef-935d-6bccd7847ba3.jpg
soldats-tirailleurs-archives.jpeg
 
Wafaransa wamefanya ukatili mkubwa sana kwa Waafrika. Hawa watu ilibidi tusiwe hata na uhusiano nao kabisa au tuwadai fidia kubwa sana kwa uovu waliofanya na wanaoendelea kuufanya kwa Afrika
 
Sehemu yoyote pakiwa na mkono wa Mfaransa amani lazima ikosekane.
 
Back
Top Bottom