Mauaji ya walinda usalama ndio mkondo mpya nchini Kenya.

Mauaji ya walinda usalama ndio mkondo mpya nchini Kenya.

Bin Adam

New Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
4
Reaction score
1
Bila shaka nyote mmesikia kuhusu vurugu na mauaji yanayoendelea huko Garissa, nchini Kenya. Japo nakashifu tendo la wanajeshi kuwavamia wakaazi wa eneo hilo, nasikitika kuwa huo ni mwiba wa kujiletea. Ni juzi tu ambapo wanajeshi hawa walirejea kutoka Somalia walipokuwa wameenda kupigana na Al Shabaab, sababu kubwa ikiwa kuilinda nchi ya Kenya. Wengi wao walipoteza maisha yao katika vita hivyo nchini Somalia. Itakuwaje basi Wakenya (wakaazi wa Garissa) kuwaua manusuru hawa? Haiwezekani wanajeshi kuuawa nje ya nchi wakiwa katika harakati ya kuilinda nchi yao na vilevile kuuawa warejeapo ndani ya nchi na wananchi wenzao. Jambo hili linahuzunisha zaidi ukizingatia kwamba ni juzi tu ambapo takriban polisi arobaini waliuawa huko eneo la Baragoi.

Mauaji haya ya polisi na wanajeshi lazima yakome. La sivyo, walinda usalama wataendelea kulipiza kisasi na wananchi wasio na makosa ndio watakaoumia.
 
Back
Top Bottom