Mauaji ya Watanzania Afrika Kusini

Jamani hapa tunawaadhibu RSA au tuiadhibu URT maana haya makampuni yameajiri vijana wengi kuliko waliokwenda south africa, yanalipa kodi na mengineyo, je wakati mnaandaa hii petition mlifiria hivyo vitu.
 
Makampuni yanayozungumzwa karibu yote yanamilikiwa na wazungu wa Afrika kusini. sasa kuyasusia makampuni haya hakusaidii kumwazibu mwafrika mzawa (Ngozi Nyeusi wa Afrika Kusini) ambaye ndie mshiriki mkuu wa mauaji ya Watanzania walioko kule.

Njia nzuri nionavyo mimi ni kwa serikali yetu kuwakumbusha wenzao wa Afrika kusini jinsi watanzania tulivyojitoa muhanga kwa ukombozi wao, Ili nao wawakumbushe wananchi wao kama wamesahau. Suala la watanzania kutokwenda kuishi Afrika kusini iwe kikazi au kwa jinsi yeyote nyingine haliwezekani kwani dunia ya sasa ni kama kijiji kidogo kisicho na mipaka. Kuna watanzania katika nchi karibu zote za Afrika wakitafuta maisha. Wapo DRC, wapo Rwanda, wapo Angola, wapo kenya, wapo Misri n.k Huwezi kudai eti wanakwenda kufanya nini Afrika kusini na ukakaa kimya kama hao hao watanzania wanaishi Nigeria au Msumbiji.

Njia nyingine ni kuwashughulikia kwa jinsi yeyote.... kuwafukuza Waafrika kusini wazawa katika nchi yetu ili wakahadithie kwao! Tunao wengi katika taasisi hizo zilizotajwa... Let them go!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…