Mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi ni janga kwa sasa. Nini kifanyike?

Mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi ni janga kwa sasa. Nini kifanyike?

haha

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
1,400
Reaction score
1,638
Kwakweli ukiwa ni msomaji magazeti na mitandao ya kijamii na vyanzo mbali mbali vya taarifa lazima utastuka hali imekua mbaya wandugu? Kulikion Watanzania! Nini kimezikumba hizi ndoa au haya mahusiano?

Mbaya zaidi mpaka watu wenye umri mkubwa wameingia kwenye mkumbo huu!

Hali ni mbaya mno tena kuna matukio mengine hayaripotiwi kabisa yaniashia chinichini. Kuuwana kuumizana kuharibiana Mali kwa watu wenye mahusiano kunatisha kwa sasa.

Tatizo ni nin!? Mbaya zaidi mauaji haya huwatesa sana watoto wanaoachwa. Mfano Mama au mke anamuua baba/mume. Mama kwenda jela baba anazikwa watoto ni wadogo. Kweli inaumiza sana?

Kuna haja ya kutafuta au kuanzisha vitengo watu wapewe elimu pindi mahusiano yanapo legalega mhusika aripoti ili ushauri ufanyike kwa walengwa.
 
Haya mambo yako kihisia zaidi.

Kikubwa ni kuushinda moyo.

Ukiona mko kwenye mahusiano,ndoa hamuelewani kila mtu achukue 50 zake.

Ova
 
Kwa interval naona kila baada ya siku mbili nakuta taarifa izo sema sisomi napitia juu juu ni janga sana😥😥😥leo nimeiona pia sijui mume amuua mke ikihusishwa na wivu wa mapenzi
 
Maadili ya ndoa yameshuka mno, wanandoa hawafuati viapo vya ndoa walivyoapa na kusaini, wanasalitiana tu. Yule anayesalitiwa hawi mvumilivu anachukua uamuzi mgumu wa kukatisha uhai wa mwenzake.

Msisitizo uwepo wakati wanafunga ndoa wajihadhari na hatari zinazoweza kutokea katika ndoa, kila mmoja aheshimu mapatano na maagano ya ndoa, yaheshimiwe na watu wote
 
Kwakeli ukiwa ni msomaji magazeti na mitandao ya kijamii na vyanzo mbali mbali vya taarifa lazima utastuka hali imekua mbaya wandugu!? Kulikion Watanzania...
Endeleeni kuwapenda mtanyooshwa hadi akili ziwakae sawa,mkiuana tunafukia..

Binafsi Siwezi ku date na mwanamke Mwenye wivu wa kipumbavu
 
Elimu ya Mahusiano na Ndoa ifundishwe Shule za Sekondari.

Hasa Form 3-4...

Vijana wajulishwe mapenzi ni mazuri ila yana misukosuko sana.

Na wajulishwe wasiue heri watengane
 
Back
Top Bottom