Mauki: Kwako Mrisho Mpoto

Mauki: Kwako Mrisho Mpoto

Makuku Rey

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
3,497
Reaction score
3,823
Kwako mrisho mpoto,
Imekuwa ni muda sasa toka tukupe nauli,pengine tingo alikupitiluiza kituo.
Maana umepita muda sasa,pengine uliogopa kushuka kwa sababu kulikuwa na mvua tena ya mafuriko ya damu na nyama.
Kama umepitiliza,ukifanikiwa kukutana na mwanzilishi wa taifa au mzimu wake.
Mwambie ile nyumba aliyoiacha yenye vijana wavivu,sasa ina vijanana wachapakazi na waoga.
Na sasaivi wanaogopa zaidi ushuru na makoro.
Msisitizie zaidi huyu baba wa kambo ameshindwa kutunza kitabu chake,amefuta sehemu za aya zake tena kwa damu.
Kibaya zaid njaa imetamalaki ndani ya nyumba,mpaka ng'ombe wanakula udongo.
Mashamba yote yamewekwa uzio,watu wamehamia shamba moja liliachwa wazi ili kunusuru matumbo yao.
Mwambie huku wameibuka wadudu wapya na wanakula mazao ya aina moja tuu
Mwisho kabisa koroboi tuliyokuwa nayo imeisha mafuta na kidumu tulikupa ww mpoto ukawekea maji ulipoondoka.
By Mauki J.S

copied&by [HASHTAG]#Makuku[/HASHTAG]
 
Naona tulikosea kumuamini Mpoto hata tukamchangia nauli na kumtuma, kumbe anatabia za kunguru, kunguru alitumwa na Nuhu kwenda kutizama nje ya Safina kama mafuriko yameisha, akahamia hukohuko kula mizoga. Huenda Mpoto amepata mzoga na tukumbuke mwenye shibe hamjali mwenye njaa.
 
Alienda kumsalimia mjomba hajarudi
 
Unapom quote mtu ni vema ukaweka link ili tuhakikishe ni yeye.
Vinginevyo nini kitatufanya tusiamini ni uzushi kama ambavyo imekuwa kawaida hapa jf
 
Back
Top Bottom