Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAULID YA AL JAMIATUL ISLAMIYYA FI TANGANYIKA MIAKA YA 1940
Nimekumbuka wakati wa utoto wetu Maulid ya Mfungo Sita iliyokuwa ikisomwa Mnazi Mmoja.
Mchana wake kunakuwa na karamu mbele ya Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na mtaa unafungwa na na majamvi yanatandikwa mtaa mzima.
Watoto wote tunakusanyika hapo na tunawekwa sehemu yetu maalum.
Miaka mingi imepita kilichobaki ni kumbukumbu nzuri katika fikra zetu.
Nimeingia katika kitabu cha Abdul Sykes kuangalia nimeandika nini kuhusu Maulid na hayo hapo chini ndiyo niliyokutana nayo.
''Baada kuunda African Association mwaka wa 1929, mwaka 1933 Kleist Sykes na baadhi ya rafiki zake wengine walianzisha Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Association of Tanganyika).
Hawa waasisi wa Al Jamiatul Islamiyya baadhi yao walikuwa wajumbe katika Kamati ya Maulidi ya Dar es Salaam.
Kleist alikuwa mwanakamati kuanzia mwaka wa 1926 na akadumu ndani yake hadi mwaka 1940 alipojitoa kwa ajili ya matatizo yaliyozuka.
Kisa hiki tutakieleza hapo baadae.
Hii ilikuwa kamati iliyowakusanya watu maarufu wa mji wa Dar es Salaam.
Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kutayarisha maulidi ya kila mwaka ya kusheherekea kuzaliwa kwake Mtume Muhammad, (Rehema na Amani Iwe Juu Yake).
Sherehe hizi zilikuwa muhimu sana hasa katika miji ya Kiislam iliyoko pwani kama, Lamu, Mombasa, Tanga, Pangani, Mikindani, Kilwa, Mtwara na Lindi.
Waislam kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki kuanzia Barawa, Somalia walialikana katika miji hii ya Kiislam kuja kusheherekea kuzaliwa kwa Mtume (SAW).
Shariff Salim Omar, liwali wa Dar es Salaam akachaguliwa kuwa rais wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Maulid Committee ilikuwapo kabla ya African Association, 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.
Waasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika walikuwa Kleist Sykes, Ali Jumbe Kiro aliyekuwa Mweka Hazina, Maalim Popo Saleh, Idd Tosiri na Mzee bin Sudi, Shariff Salim Omar kwa kuwataja wachache.
Hii ilikuwa miaka ya 1930 kwenda miaka ya 1940 na mji wa Dar es Salaam ulikuwa na siasa zake maalum ndani ya ukoloni wa Muingereza khasa baada ya kumalizika kwa Vita Vya Pili Vya Dunia.
Tuanze na Liwali wa Dar es Salaam Ahmed Saleh.
(Miaka mingi sana baadae nilikuja kusoma na wajukuu zake St. Joseph's Convent na miaka mingi baadae baada ya kumaliza shule na kwa kweli ni mwezi uliopita nilikutana na mjukuu wake mwanamke na kutambulishwa kwani nilimsahau.
Nilifurahi kukutana na ''school mate,'' baada ya miaka 50.
Miaka mingi alihama Tanzania.
Lakini kilichonifurahisha zaidi ni pale nilipomsikia anazungumza Kiingereza safi wala hakina mfanowe.
Tulipoagana nikawa najiambia, ''Hawa wajukuu wa Liwali Ahmed Saleh matata kama babu yao.''
Ndugu yake wa kiume kwa miaka mingi yuko Ulaya na ni mwanamuziki mkubwa anaepiga piano na kuimba kwa ustadi mkubwa sana.
Inataka uone video zake ndiyo utaelewa ninachokueleza.
Liwali Saleh alikuwa Mwarabu na Tewa Said Tewa aliniambia kuwa alipenda mno madaraka na ukubwa.
Yeye alitaka kila jambo la Waislam na khasa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lianzie na kumalizikia kwake.
Liwali Ahmed Saleh alikuwa na uhusiano mzuri na Waingereza.
Sasa tuje kwa Sheikh Ali Saleh.
Wakati ule Sheikh Ali Saleh Mwarabu vilevile kama alivyokuwa Liwali Ahmed Saleh, ndiye alikuwa rais wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Halikadhalika Sheikh Ali Saleh alikuwa Imam wa Msikiti wa Ijumaa ukijulikana kwa jina maarufu, Msikiti wa Kitumbini.
Sheikh Ali Saleh alikuwa mtu shujaa asiyeogopa mtu.
Wakati ule wa ukoloni bila woga wowote alikuwa akitoa khutba za hamasa katika sala ya Ijumaa akiunga mkono Waarabu wa Palestine dhidi ya Wayahudi.
Halikadhalika wakati ule kuliwa na suala la mitaala ya shule.
Vitabu vya kiada vilivyokuwa vikitumika shuleni vilikuwa vimejaa propaganda dhidi ya Uislam.
Katika vitabu hivyo Uislam ulionyeshwa katika sura ya kuleta utumwa Afrika.
Vitabu vilieleza kuwa Uislam ulienezwa kwa nguvu ya upanga.
Sheikh Ali Saleh na Al Jamitul Islamiyya fi Tanganyika hawakukubaliana na uongo huo na hiyo ndiyo ikawa sababu ya mapambano baina yao na serikali.
Serikali iliona Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ilikuwa sasa inajiingiza katika siasa.
Serikali kutaka kuikomesha Al Jamiatul Islamiyya ikawa inatafuta sababu ya kuifunga shule yao.
Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kwa wakati ule ilikuwa ikishughulika na kuendesha shule na kusoma Maulid ya Mfungo sita.
Nguvu ya Waislam katika Tanganyika ikawa inaonekana katika mikusanyiko ya Maulid kuanzia kwenye karamu mchana na jioni baada ya Sala ya L'Asr katika zafa katika mitaa na barabara za Dar es Salaam.
Wake kwa waume na watoto walitoka kushiriki katika zafa.
Mji ulipambwa na ukapambika.
Hamasa hii ndiyo iliyokuwako pale kilipoundwa chama cha TANU kudai uhuru wa Tanganyika.
Inaweza ikaendelea In Shaa Allah...au hii ikawa ndiyo tamati.
PICHA:
Kulia Sheikh Said Chaurembo na Liwali Ahmed Saleh.
Sheikh Ali Saleh.
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika linavyoonekana hivi sasa katika Mtaa wa Max Mbwana (Stanley Street).
Hija 1964 waliosimama wakwanza kulia Abdul Sykes, Tewa Said Tewa na waliokaa wa kwanza kushoto ni Chief Abdallah Said Fundikira.