Maumivu chini ya kitovu

ntamaholo

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
12,938
Reaction score
6,942
Salam ndugu zangu.

Mke wangu ni mjamzito wa miezi minne japo unaenda mwezi wa tano. Mimba alinasa january, wkt bado hajaconferm, akapatwa na malaria, alipima akaamua kumeza malafin/metacafrine.

Mwezi wa pili hali ilimrudiia ya ugonjwa akapimwa akakutwa na malaria na dk kwa kuwa alimpima na mimba na alipopewa historia fupi, alisema ni kosa kubwa kumeza metacafrine ukiwa na mimba changa hivyo yeye akamshaur ameze aidha sp au amodiaquin. Wife akachukua amodiaquin akapata nafuu kidogo.

Mwezi wa tatu afya ikayumba tena, tukarudi kwa dr wa awali hatukumkuta, tulikutana na dr mwingine, akampima akakuta tena makaria, safar hii wife akaona atumie SP. Lkn bado hakupona. Baada ya kumaliza doz hali ikawa mbaya zaidi hivyo tukaenda hospital ya wilaya tena tukaanzia clinick.

Tulieleza tangu mwezi wa kwanza hadi huo wa nne na dawa alizomeza. Alipima malaria akakutwa na tatu wkt awali zilikuwa moja tu. Hivyo dr akashaur alazwe ili quinin itumike. Quinini ilitumika na baada ya doz kuisha akasikia afya imerejea, tukafurahi.

Baada ya wiki mbili tangu atumie quinin, kwa siku mbili alitokwa na majimaji uken lkn baadae yalikoma kutoka.

Sasa huu wa tano umekuja na mapya. Kila asubuhi lzm atapike. Hahisi homa wala kichefuchefu lkn anatapika kweli hadi siku moja akatapika vitu kama damu.

Mbaya zaidi, ameanza kuhisi uzito kwenye kinena chini ya kitovu na kwa maumivu anayodai kuyapata, anasema ni mithili ya eneo la mwli ambalo LIMETUNGA USAA NA LINATAKA KUPASUKA ILI USAA UTOKE. Ndiyo maumivu ayapatayo.

Tunapanga kurudi kwa dr wa mama na mtoto, naombeni ushauri wenu ili tujue la kufanya pia.

Nb. Miez minne hajawahi kusikia kitoto kikicheza, ila tumbo linakuwa kwa kasi tu.
 
Quickening au mtoto kucheza inategemea na sensitivity ya mama husika lakini wengi huanza kusikia kuanzia wiki ya 18-20. Na kuhusu maumivu chini ya kitovu yawezekana ana uambukizo kwa njia ya mkojo
 
Quickening au mtoto kucheza inategemea na sensitivity ya mama husika lakini wengi huanza kusikia kuanzia wiki ya 18-20. Na kuhusu maumivu chini ya kitovu yawezekana ana uambukizo kwa njia ya mkojo

aksante kwa neno lako. inabidi waeende naye clinic ya mama na mtoto wapime wote maana magonjwa ya kuambukiza yapo mengi sana na baadhi yasipodhibitiwa huweza kuleta madhara makubwa.
 
Quickening au mtoto kucheza inategemea na sensitivity ya mama husika lakini wengi huanza kusikia kuanzia wiki ya 18-20. Na kuhusu maumivu chini ya kitovu yawezekana ana uambukizo kwa njia ya mkojo
Nyalotsi ubarikiwe. Pia ntagunga aksante kwa ushauri. Inabidi tuwahi kwa dr maana duh usingizi kuna kipindi unagoma!

N
 
Nyalotsi ubarikiwe. Pia ntagunga aksante kwa ushauri. Inabidi tuwahi kwa dr maana duh usingizi kuna kipindi unagoma!

N

Usisahau kumpa support ya kutosha kwa kipindi hiki! Wanaume wengi ndio wanakimbiliaga kwenye michepuko wake zao wanapokuwa wajawazito. Mkeo anahitaji uwepo wako kimwili na kiroho!
 
Usisahau kumpa support ya kutosha kwa kipindi hiki! Wanaume wengi ndio wanakimbiliaga kwenye michepuko wake zao wanapokuwa wajawazito. Mkeo anahitaji uwepo wako kimwili na kiroho!
Aksante kwa ushauri. Namshukuru Mungu kuwa tangu nianze maisha ni mke wangu 2011, michepuko imekuwa si vipaumbele vyangu
 
rud hosp lakini hakikisha anafanyiwa vpimo kama ultrasound kucheki mtoto kama yuko alive , urinalysis au urine c/s kucheki kama ana u.t.i , widal test kama ana typhoid, arudie kucheki malaria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…