Jamani naombeni msaada ninajisikia maumivu kwenye shingo sasa ni wiki ya tatu bado hayajaisha. Mwanzoni nilidhani labda kulala na mto nikaacha ila bado maumivu yakaendelea nikaenda kucheck malaria wakaniambia nina malaria nikanywa dawa nikamaliza ila bado nasikia maumivu. Sasa hivi kuna jamaa zangu wawili nao wanajisikia maumivu kama yangu. Naombeni msaada wa matibabu au kama kuna mlipuko wa ugonjwa na matibabu yake ni yapi?