Maumivu kwenye tumbo au mbavu (wengi huita vichomi)

Maumivu kwenye tumbo au mbavu (wengi huita vichomi)

SSMashinji

Senior Member
Joined
Aug 10, 2023
Posts
129
Reaction score
191
VICHOMI ni lugha ilio zoeleka kwa wanao sema kua kuna vitu vinachoma juu ya tumbo au mbavu, maumivu makali na ya mda mfupi kama mwiba umechoma eneo kilo.

LAKINI KIUHALISIA TUKISEMA TUNAVICHOMI TUNA FICHA MAGONJWA MENGI KWENYE SHIDA INAYOWEZA PUUZWA NA WENGI KWAMBA "...😕.ma'''''ke iki kichomi nacho aaaaaaaaaa ..."

Lakini kwa za chinichini VICHOMI ni kama tumbo kujaa gesi fujo fujo zile za kwenye utumbo ndio vimaumivu vinatokea tumboni, tumbo full tank 24/7 n.k

THEN HAYO MAELEZO TUNAYOYAWEKA KUMAANISHA KICHOMI NI NINI maana vichomi kwa tafsiri vinatakiwa vitokee tumboni.:think3D:

Naongelea hivi vimaumivu kwenye mbavu ambavyo vinaweza kikakufanya uache kupiga story kwa heshima na taadhima ukashusha na glass ya juice mezani chap..... kwa upooole unajkunja una shka mbavu .

Ok kuna hawaapa.

1. KUKAZA AU KUVUTA MISULI KATI YA MBAVU (Intercostal Muscle Strain) -> husababishwa na kazi tu za kawaida za cku zote, kucheka au kukohoa kwa nguvu, ajali kifuani au kuangukia kifua, tumbo kujaa gesi.

Kinga ni bora kuliko tiba: kupasha misuli ya mgogo na kifua kwanza kabla ya mazoezi, kufanya mazoezi ya kuimalisha misuli, kua na mkao mzuri wakati wa kukaa au kufanya kazi, kuepuka kugeuka ghafra pia kunyanyua vitu vizito bila maandalizi.

2. PLEURODYNIA, au devil's grip pia inadalili hizo hizo zilizopewa kichomi, lakini sababu yake hua ni athari au maambukizi ya virusi vinavyoathiri misuli ya kifua(hasa Coxsackie B) Husambaa kwa maji,vyakula au majimaji ya mtu alie na virusi hivi mfano mate. etc

Dalili za ziada ni mda wa maumivu kuongezeka kwa haraka mda wa kupumua kwa nguvu, kukohoa au kusogea, vihoma +uchovu+ maumivu ya kichwa.

Ni vyema kupima kama vipimo vipo ila kwa kutuliza maumivu kua mteja wa ibuprofen.

3. KUVIMBA KWA CARTILAGE INAYOUNGANISHA MBAVU NA MFUPA WA KIFUA(Costochondritis) hamna maelezo hapa utajua tu baada ya kuhangaika mda mrefu na utakumbuka kwenda checkup.

4. Pneumothorax (Collapsed lungs) pia utajua tu baada ya kuteseka sana bila checkup yoyote.

5. Gallstones( Mawe kweye kibofu cha mkojo) maumivu kidogo hapa yamekaa upande mmoja juu ya tumbo upande wa kulia na yanaweza kuenea hadi kwenye mbavu au mgongo.

6. BONUS UGONJWA, KIDOLE UTUMBO KUHARIBIKA pia imekaa kama kichomi ila ni upande mmoja pia kulia chini, ni story ndefu kwakua haka kakiungo kamenifanya nipigwe full kaputi 12hour vijeba wanahangaika na utumbo wangu.

and GOD knows why aka kadude haijulikani kanafanya kazi gani kwenye mwili wa binadamu zaidi ya kutunza bacteria wazuri ...dadek..🦧

NI KWAMBA HAMNA UGONJWA MDOGO HATA MAFUA AMBAYO TUNAYAMUDU BONGO MAMBELEE YANAWAUA
kama nimekosea chochote kumradhi, am not an Angel
 
Back
Top Bottom