Maumivu wakati wa kukojoa

wayzee

Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
47
Reaction score
40
Nina mzee wangu kanipigia simu anasema akitaka kukojoa mpaka ajikamue sana na mkojo unakuwa kama hautoki then anapata maumivu makali sana na anajiskia kukojoa mara nyingi kiasi ameshindwa ata kwenda kazin maana yupo jirani na kopo la mkojo...

Umri ni miaka 57 na tatizo limeanza jana.

Msaada tafadhali
 
Awahi hospitali labda ana dalili za TEZI DUME
 
Ni tezi dume limeanza kuziba njia ya mkojo awahi hospitali otherwise atashindwa kojoa kabisaaa. Akacheki na UTI maana hiyo obstruction Mara nyingine huchagiza ukuaji Wa bacteria. Muulize ili kuthibitisha....je anahisi akikojoa mkojo hauishi yaani unabaki ndani? Je urefu wa kutupa mkojo umepungua? Yaani kale kaumbali kutoka alipo hadi unapotua mkojo; je anavujisha mkojo baada ya kumaliza mpaka chupi au boksa kuloa? Je analoesha hadi viatu sometimes akikojoa. Akijibu ndio nakupa asilimia 70 itakua yenyewe. Kila la khair
 
Wahi hospital mkuu kabla haujawa chronic na kuanza kutumia mirija.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…