Maumivu ya jino

mikumiyetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Posts
1,312
Reaction score
944
Mmeamkaje wandugu usiku mzima leo sijalala kwa raha kutokana na maumivu ya jino, jino lenyewe limetoboka. Ushauri wenu nikienda kuliziba maumivu yataisha au nikaling'oe tu?
 
Mmeamkaje wandugu usiku mzima leo sijalala kwa raha kutokana na maumivu ya jino,jino lenyewe limetoboka.Ushauri wenu nikienda kuliziba maumivu yataisha au nikaling'oe tu?
Kaling'oe mkuu, ukiziba maumivu yatapungua lakini baada ya muda yatarudi tena.
 
Nina magego mawili yametoboka moja juu na jingine chini. Gego moja limemeguka vipande upande mmoja lishaisha na gego la chini limetoboka na huu ni mwaka wa pili napeta nayo nakula chochote pasipo maumivu yeyote.

Dawa niliyotumia ni mkojo wangu ulionitibu.

Nakushauri uamkapo nawe asubuhi mkuu mkojo wako wa kwanza kabla yakuweka chochote mdomoni , sukutua kwa mkojo wako huo kwa muda wa dk 5 kwa siku 3 mpaka 5 hakika tatizo litakwisha.

Unaposukutua jitahidi kuuzungusha mkojo katika kinywa kila sehemu. Ukimaliza unatema baada ya dk 10 safisha kinywa kwa mswaki na dawa.
 
Dhuu asante mkuu kwa ushauri
 
Kama limetoboka bora ukalitoe huwa kuna wadudu wanashambulia hapo kwasababu kuna mabaki ya chakula huwa yanabaki kwenye kishimo na baadaye kinywa huanza kutoa harufu mbaya.
 
Kama limetoboka bora ukalitoe huwa kuna wadudu wanashambulia hapo kwasababu kuna mabaki ya chakula huwa yanabaki kwenye kishimo na baadaye kinywa huanza kutoa harufu mbaya.
Asante nimetoka hospital sasa kulitoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…