maumivu ya kichwa

Ledisia

Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
10
Reaction score
0
wapendwa mwenzenu kichwa kinaniua jamani nimetumia dawa bila kupona naombeni ushauri nn tiba mbadala
 
wapendwa mwenzenu kichwa kinaniua jamani nimetumia dawa bila kupona naombeni ushauri nn tiba mbadala
maelezo yako hayajitoshelezi. Elezea kinavyouma kwa ufasha. Huwezi, nenda kamuone daktari
 
kapime ujue una tatizo gani. . .kama hutakuwa na ugonjwa wowote basi punguza mawazo,jipe mda wa kurelax au ukapime macho!
 
Labda macho yana shida,nenda hospital.
 
wapendwa mwenzenu kichwa kinaniua jamani nimetumia dawa bila kupona naombeni ushauri nn tiba mbadala


Maji huzuia na kuponya kabisa maumivu mbalimbali mwilini:


Ishara za mwanzo kabisa za asidi kuunguzwa ndani katikati ya seli au kwa maneno mengine asidi kuzidi kwenye seli za mwili na madhara ya kijenetiki ambayo yanaweza kujionesha, ni maumivu mbalimbali yanayozidi kujitokeza katika mwili.

Kutegemea na kiasi cha upungufu wa maji mwilini na namna na eneo lenyewe asidi ilipojijenga (ambayo ingeondolewa kwa kuongeza kunywa maji tu), maumivu maalumu ya mwili hujitokeza!

Maumivu hayo yanajumuisha; kiungulia (heart burn), maumivu ya moyo (angina), maumivu sehemu ya chini ya mgongo (lower back pain), yabisi (rheumatoid), maumivu ya kichwa (migraine headaches), homa za asubuhi kwa kina mama wajawazito na maumivu mengine mengi unaweza kuyataja.

Watu wengi siku hizi hawawezi kuishi bila kumeza aina fulani ya dawa ya kupunguza maumivu.
Ni rahisi kuelewa namna gani maumivu ambayo hayajasababishwa na ajari au maumbukizo yanavyoweza kujitokeza mwilini.

‘Namna hii rahisi ya namna maumivu yanavyotengenezwa mwilini imetupumbaza wengi wetu sisi katika taaluma ya madawa tangu binadamu alipoanza kutafuta suluhu ya maumivu ya mwili kwa kutumia dawa – dr Batmanghelidj'.

Viwanda vya madawa vinatumia mabilioni ya fedha kutafiti dawa hizi na zile za kuondoa maumivu na mabilioni mengine zaidi hutumika kutangaza aina fulani ya dawa za kuondoa maumivu.

Upungufu wa maji mwilini (dehydration) unaweza kutibiwa kwa kuongeza kunywa maji tena bure bila gharama yeyote.
Ili kuuelewa mfumo wa utengenezwaji wa maumivu mwilini, tunahitaji kwanza kujifunza namna usawa wa asidi na alkalini unavyofanya kazi mwilini.

Hali ya uasidi husababisha kuunguzwa kwa baadhi ya miishio ya neva mwilini. Kunapotokea hayo, ubongo huonywa juu ya mabadiliko hayo ya kikemekali ya kimaeneo, ambayo sote hutafusiri kama MAUMIVU. Kwa maneno mengine, hali ya uasidi ndani ya mwili ndiyo hupelekea sisi kusikia maumivu.

Kwa kawaida wakati damu yenye maji ya kutosha inapoizunguka seli, baadhi ya maji huingia ndani ya seli na kutoa nje molekuli za haidrojeni. Maji huisafisha asidi toka ndani ya seli na kuiacha sehemu ya ndani ya seli katika hali ya ualikalini ambayo ni hali yake ya kawaida na ya mhimu.

Kwa afya bora kabisa, mwili unatakiwa kubaki katika hali ya 7.4 katika kipimo cha ph (potential hydrogen).
Hali hii huhamasisha afya kwa sababu ndiyo hali inayoviwezesha vimeng'enya vinavyofanya kazi ndani ya seli ambavyo hupata ufanisi mzuri katika ph hii. Utiririkaji wa kutosha wa maji ndani na nje ya seli huifanya sehemu ya ndani ya seli kubaki na kuhimili hali yake ya kiafya ya kiualikalini.

Ndani ya miili yetu, figo husafisha haidrojeni iliyozidi ambayo husababisha asidi toka katika damu na kuiweka katika mkojo unaozarishwa. Kadiri mkojo unavyozarishwa kwa wingi ndivyo mwili unavyojiweka katika hali ya ualikalini kirahisi zaidi. Hii ndiyo sababu mkojo unaokaribia rangi ya uweupe ni kiashiria cha kufanikiwa kwa mfumo wa uondoaji wa asidi mwilini, wakati mkojo wa rangi ya njano au chungwa ni ishara ya kuunguzwa kwa asidi mwilini.

Watu wanaodhani kwenda uani kwa ajili ya haja ndogo mara mbili au tatu kwa siku ni usumbufu kwao na hivyo kuacha kunywa maji ili kuzuia hilo hawana uelewa wa namna wanavyohatarisha miili yao.

Ubongo unalindwa vizuri zaidi dhidi ya asidi kutokana na ukweli kuwa unapata umhimu wa kwanza katika kusambaziwa maji kwa ajili ya mahitaji yake yote. Sehemu zingine za mwili haziwezi kuwa na bahati hii wakati maji yanapokuwa yanapatikana kwa njia ya mgawo. Ingawa upungufu wa maji unapobaki kwa muda mrefu, ubongo pia huathiriwa kutokana na hali ya uasidi katika seli, hivyo hali kama za kupoteza kumbukumbu na magonjwa ya mishipa hujitokeza.
Maumivu ambayo hayakusababishwa na jeraha au ajari, ni kiashiria kuwa tishu, ogani, maungio na seli vina asidi iliyozidi ambayo inahitaji kufanywa kuwa alkalini.

Kwa kunywa glasi moja (ml 250) ya maji halisi na kuchukua kipande cha chumvi ya baharini, kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa maumivu.

Jaribu hii kwa kunywa glasi moja ya maji na kisha kuiweka chumvi mwishoni mwa ulimi wako na kuiacha iyeyuke kwa dakika na kisha isafishe kwenda chini na glasi ya pili ya maji. Kwa mjibu wa dr.Batman, kitendo hiki kitabadili PH ya damu, tishu, ogani na seli ndani ya mwili.

Ikiwa Umeipenda, Wajurishe jamaa na rafiki zako.

Makala hii imechotwa kutoka:
[url]www.maajabuyamaji.net[/URL]


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…