Benokolongokonongose
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 213
- 52
Bwana YESU apewe sifa, Asalaam aleykum. Wadau mimi nina shida. Nasumbuliwa sana na maumivu ya kiuno, tumbo na miguu. Nina mtoto mmoja mwaka mmoja na miezi kumi sasa. Na nina kipandikizi cha kuzuia mimba. Wiki iliyopita nilikwenda hospitali kumweleza daktari akasema kipandikizi ndo kinasababisha hayo yote. Nilimwambia nifanyiwe yutura saundi au xray akasema haina haja ila shida ni kipandikizi. Akaniandikia tu panadol. Muda huu maumivu ni makali sana. Sasa naomba kujua kama kipandikizi kinauhusiano na haya. ASANTENI. Wenu, Benokolongokonongose.