Maumivu ya kulea mtoto bila uwepo wa karibu wa baba yake, yasikuyumbishe kwenye maisha

Maumivu ya kulea mtoto bila uwepo wa karibu wa baba yake, yasikuyumbishe kwenye maisha

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
đź“–Mhadhara wa 22:
Ni kama zimeanza kujengeka fikra na hisia mbaya za kudhani kwamba kuwa SINGLE MOTHER ni kufeli maisha, au ni maumivu makubwa kuliko maumivu mengine yoyote hapa duniani. Kama una fikra hizo achana nazo zitakuchelewesha.

Kuna baadhi ya wanawake baada ya kujikuta wamekuwa SINGLE MOTHERS wanatumbukia kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Pengine unakuta mwingine ana kazi nzuri, biashara nzuri, n.k, lakini anajikuta anaharibu biashara yake, ajira yake, mtaji wake kwasababu kutwa yupo ndani anawaza.

Ni kweli kuna maumivu fulani ya kulea mtoto bila uwepo wa karibu wa baba yake, au labda ulidata na penzi la baba wa mtoto. Lakini hebu fikiria kama ulifika muda ukatengana na wazazi wako ukaenda kutafuta maisha pekee yako, kwanini unaharibu maisha yako kwasababu ya msongo wa mawazo ya kutengana na mtu uliyekutana nae ukubwani? - Acha maisha mengine yaendelee.

Wale mnaodhani kuwa SINGLE MOTHER ni maumivu makali sana kuliko maumivu yoyote duniani basi umefeli kufikiria, amka ufikirie tena. Hebu mtafute mwanamke mwenzako ambaye anaishi na mume (ameolewa) lakini hakubahatika kupata mtoto na hana dalili ya kupata mtoto, halafu uketi nae sebuleni ili akwambie ile hali anayopitia yeye ikoje - Hapo ndipo utagundua kwamba Mwenyezi Mungu amekupendelea kwa kukupa neema kubwa sana.

Kuhusu kuwa SINGLE MOTHER na masuala ya kiuchumi:- Usilinganishe neema ya kupata mtoto na vitu vya Mzungu ambavyo vinatafutwa. Ukishakuwa na uwezo wa kudaka ujauzito hakika mwambie Mungu "asante" kwa sababu umepata neema kubwa sana, hayo mengine ambayo bado hukuyapata yanasubiri juhudi zako na utulivu wako.

NB: "Sio lazima kuwa Single mother, lakini ikibidi; yaache maisha mengine yaendelee"

Right Marker
Dar es salaam
Sept 27, 2024.
 
Cha ajabu hapo anayedhurika ni mtoto sio mama. Stress zake au maumivu yake sio jambo la muhimu maana mwanaume aliyekutana nae na kuzaa nae ni yeye kamchagua. Mtoto hakushiriki so mateso anayopitia mtoto ndio kisanga kilipo.
 
Back
Top Bottom